Posts

Showing posts from June 19, 2019

RAISI MSTAAFU WA KONGO AKWAMA KWENYE FOLENI KAMA RAIA WA KAWAIDA HUKU AKIENDESHA MWENYEWE GARI

Image
Joseph Kabila bloqué dans un embouteillage sur l'avenue des Poids lourds à Kinshasa. L'ancien président congolais Joseph Kabila a été bloqué dans un embouteillage sur l’avenue des poids lourds ce mercredi 19 juin 2019. Il est presque 14h00 heure de Kinshasa lorsque le cortège du désormais sénateur à vie Joseph Kabila est bloqué dans un embouteillage monstre au niveau du croisement Poids lourds et avenue de la Funa dans la commune de Limete. Il était seul au volant de sa ... Tazama Zaidi    #DRC Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Joseph Kabila,alikwama katika foleni ya barabarani sur l'avenue des poids Mjini Kinshasa. ilikua siku ya jumatano hii tarehe 19/062019 kabila akiwa katika gari lake akiendesha mwenyewe na mlinzi wake na nyuma kukiwa na gari nyingine Range lover ikimsindikiza na mlinzi mmoja alisimama kwenye foleni kama raia wengine. Watu walijaa kumshangilia huku wengine wakisikia wakimpongezaa na kusema kuna maisha baada ya uchaguzi na Rais

ELEWA

Image
Kama ukijaribu kuzuia Chafya, unaweza kuharibu mfumo wa mapafu, macho kupasuka, ngoma za sikio kupasuka na mishipa ya damu sababu ni Presha kubwa inayobaki ndani inatafuta sehemu za kutokea.

KIPAJI

Image
MUNGU HAMTUPI MJA WAKE: Licha ya ulemavu alionao mtoto Anzilan Mayani mkazi wa Ilolo wilayani Mbozi mkoani Songwe, amekuwa akishangaza watu wengi kutokana na kipaji alichonacho ukizingatia hajawahi kupata elimu yoyote. Anzilan ni binti mwenye umri wa miaka 14, licha ya kuwa na ulemavu huo ambao umepelekea kutojiweza kwa lolote bado Mwenyezi Mungu amempa kipaji cha kuchora kwa kutumia miguu bila kufundishwa na mtu yeyote bali kwa kupitia picha anazoziona kwenye magazeti ama kw a kumuangalia mtu. Kutokana na kutoweza kufanya jambo lolote, imekuwa vigumu kwake kupata fursa ya masomo kutokana na kukosa watu wa kumuhudumia na hivyo kuishia kukaa nyumbani tu.

MHANDISI AJINYONGA KWA KUTUMIA SURUALI YAKE

Image
MBEYA: MHANDISI AJINYONGA KWA KUTUMIA SURUALI YAKE > Aswile Msika (37) Mhandisi wa Halmashauri ya Chunya ajiua kwa kujinyonga katika eneo la Nyatura Kata ya Mbugani > Alikuwa akituhumiwa kwa kuomba na kupokea rushwa

NANI MUOVU ZAIDI KATI YA MUACHA SWALA NA MZINIFU?

. NI YUPI ANA HATARI ZAIDI MBELE YA ALLAH, MZINIFU AU MUACHA SWALA?! أَنَّ أَبَا ذَرٍّ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ حَدَّثَهُ، قَالَ : أَتَيْتُ النَّبِيَّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ وَعَلَيْهِ ثَوْبٌ أَبْيَضُ، وَهُوَ نَائِمٌ، ثُمَّ أَتَيْتُهُ وَقَدِ اسْتَيْقَظَ، فَقَالَ : " مَا مِنْ عَبْدٍ قَالَ : لَا إِلَهَ إِلَّا اللَّهُ. ثُمَّ مَاتَ عَلَى ذَلِكَ، إِلَّا دَخَلَ الْجَنَّةَ ". قُلْتُ : وَإِنْ زَنَى وَإِنْ سَرَقَ ؟ قَالَ : " وَإِنْ زَنَى وَإِنْ سَرَقَ ". قُلْتُ : وَإِنْ زَنَى وَإِنْ سَرَقَ ؟ قَالَ : " وَإِنْ زَنَى وَإِنْ سَرَقَ ". قُلْتُ : وَإِنْ زَنَى وَإِنْ سَرَقَ ؟ قَالَ : " وَإِنْ زَنَى وَإِنْ سَرَقَ عَلَى رَغْمِ أَنْفِ أَبِي ذَرٍّ ". وَكَانَ أَبُو ذَرٍّ إِذَا حَدَّثَ بِهَذَا قَالَ : وَإِنْ رَغِمَ أَنْفُ أَبِي ذَرٍّ. (متفق عليه) Abuu Dharr amehadithia kuwa 'Nilimwendea mtume wa Allaah nikakuta amevaa nguo nyeupe mno hali ya kuwa amelala (Nikamwacha) Kisha nikamwendea tena hali kashaamka akasema *"Mja yeyote atayesema لا إ

HABARI

Image
Ndugu 4 wafamilia moja akiwemo Bibi harusi wamefariki Dunia alfajiri ya leo kwa ajali ya gari karika eneo la Machimbo Mbeya, wakati wakielekea DSM kwa maandalizi ya harusi, waliofariki ni Diana Mwandunga (Bibi Harusi), Faraja na James Mwandunga, na mtoto Janton.

MICHEZO

Image
KIBO BOYS WAENDELEA ‘KUSHIKILIA VIFAA’ VYAO Klabu ya KMC imemsajili rasmi mchezaji Ismail Gambo kwa mkataba wa miaka mitatu utakaomalizika mwezi Juni mwaka 2022. Gambo alikuwa KMC kwa mkopo kutoka Azam FC na sasa ni mchezaji rasmi wa timu hiyo yenye jukumu la kuiwakilisha Tanzania kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika msimu ujao. Klabu hiyo pia imewaongezea mikataba wachezaji wake Rehani Kibinga na Sadala Lipangile waliosaini mikataba mipya ya miaka mitatu kila mmoja hadi mwaka 2022.

HUKO ELDORET KENYA MWANAUME AMEWEKWA MAHABUSU YA KIKE WAKIDHANI MWANAMKE

Image
Kizaazaa: Mwanaume ashikiliwa kwenye Gereza la wanawake Sambaza habari hii Facebook   Sambaza habari hii Messenger   Sambaza habari hii Twitter   Sambaza habari hii Email   Haki miliki ya picha MWANANCHI Kulikuwa na hali ya mshtuko katika mahakama moja mjini Eldoret siku ya Jumanne baada ya kubainika kuwa mshukiwa aliyekuwa akishikiliwa kwenye gereza la wanawake ni mwanaume. Mshukiwa huyo anayetambulika kwa jina Shieys Chepkosgei siku ya Jumatatu alikamatwa katika Chuo na Hospitali ya Rufaa ya Moi ambapo alikua akifanya kazi kama muuguzi mwanafunzi wa kike ingawa hakusajiliwa hapo. Baada ya kushtakiwa, alipelekwa kwenye gereza la wanawake la Eldoret kusubiri maamuzi ya mahakama huku akitambuliwa kama mwanamke.Gazeti la Daily Nation la Kenya limeripoti. Hatahivyo, siku ya Jumanne askari magereza katika ukaguzi wao wa kawaida waligundua kuwa mshukiwa alikua mwanaume. Uchunguzi wa haraka ulifanyika kubaini ukweli kabla ya kufanyiwa vipimo ili kujihakikishia j

MAARIFA

Image
Picha hii ilipigwa mwaka 2013 katika mbuga ya wanyama ya Maasai Mara, nchini Kenya na mpiga picha za wanyama (wildlife photographer) Alison Buttigieg, na ilishi nda kuwa picha bora ya mwaka katika tuzo za habari huko Australia. Swala huyu anayesulubiwa na chui hawa, ni Mama wa watoto wawili. Akiwa na wanae kwenye maskani yao, walivamiwa na chui waliokuwa na njaa. Watoto wake walikuwa wadogo na hawakua na nguvu za kuweza kukimbia na kujiokoa. Mama yao angaweza kuaamua kukimbia na kuwaacha wanae ambao wangeweza kuwa chakula cha chui. Lakini hakuwaacha alikimbia nao. Baada ya umbali kidogo akaona chui wamemkaribia. Akaacha wanae waende na yeye akapunguza mwendo. Alitaka kuhakikisha wanae wanakuwa salama hata kama yeye atadhurika. Chui wakamfikia na kumparamia. Katikati ya chui wawili bado aliweza kusimama wima na kuwatazama wanae ambao walikuwa wakizidi kuyoyoma porini. Alikuwa akiwatazama kwa mara ya mwisho maana alijua hatawaona tena!!! Ilikuwa ishara ya kuwaaga.