Posts

Showing posts from December 7, 2019

HISTORIA KWA UFUPI

Image
Msikiti Mtukufu wa Makka, huu ni msikiti mkongwe ambao kiasili kabisa ulianza kujengwa (kuwekwa msingi) na Nabii Adamu (Adamu huyu tunaemjua baba wa watoto wa Adamu na mume wa mama yetu Hawa ) na baada ya karne nyingi kupita ulikuja kujengwa upya na Nabii Ibrahimu akishirikiana na mwanae Ismail toka hapo ukaendelea kuboreshwa kadri teknolojia zinavyokua na mahitaji ya watu kuongezeka. Hii ni nyumba ya ibada inayobeba watu wengi kwa wakati mmoja kuliko nyumba za dini zote duniani kwani huingiza karibu watu milioni tatu kwa mara moja. Ibrahimu alikuwa na watoto wawili, Ismail kwa mkewe mdogo(hajra) ambae huyu Ismail kizazi chake ndio baadae alikuja kuzaliwa Nabii Muhammad Swalallah alayhi wasalama, na Is'haka kwa mke mkubwa ambae awali hakuwa akizaa mpaka akamuamuru mumewe aoe ili wapate mtoto baada ya mumewe kumuoa kijakazi wake Allah akaleta miujiza yake huyu mama Sara akashika mimba akiwa na zaidi ya miaka sabini, na hii ilikuwa baada ya Hajra (mke mdogo kupata