UTURUKI YANUNUA SILAHA HATARI ZAIDI DUNIANI KUTOKA URUSI
Uturuki kununua mfumo wa kujilinda dhidi ya makombora wa S-400 kutoka Urusi licha ya pingamizi ya Marekani Sambaza habari hii Facebook Sambaza habari hii Messenger Sambaza habari hii Twitter Sambaza habari hii Email Haki miliki ya picha GETTY IMAGES Image caption Mfumo huo wa S-400 ni mojawapo wa silaha kali ya ardhini dhidi ya makombora Rais wa Uturuki Reccep Tayyep Erdogan amesema kuwa ana matumaini kwamba mfumo wa kujilinda dhidi ya makombora wa Urusi ambao Washington unauona kama tishio kwa ndege za Marekani utawasilishwa nchini humo mwezi Julai. Marekani imesema kuwa Uturuki haiwezi kuwa na mfumo huo wa S-400 pamoja na ndege za kivita za Marekani aina ya F-35. Lakini bwana Erdogan amesema kuwa Uturuki itamwajibisha mtu yeyote atakayeiondoa kutoka kwa mpango huo wa ununuzi wa ndege za F-35 Uturuki ambayo ni mwanachama wa Nato imetia asaini ya kununua ndege 100 aina ya F-35 na imewekeza vya kutosha katika mpango huo wa F-35. Kampuni ...