Posts

Showing posts from July 17, 2019

HISTORIA YA KHALIFA WA PILI SAYYIDNA OMAR (R.A)

HISTORIA YA KHALIFA WA PILI SAYYIDNA OMAR (R.A) Omar bin Khatab alizaliwa mwaka 583 A.D ,asili ya familia yake inatokna na kabila LA Kikureish ..Katika ujana w ake Omar alikuwa maarufu ktk upiganaji .Baadhi ya wanahistoria wa kiislam wanasema Omar (r.a) alikuwa ni miongoni mwa watu wachache waliokuwa wanajuwa kusoma na kuandika ktk Mji wa Makka kabla ya kuja Uislam . Kazi yake kubwa ilikuwa ni biashara .Wakati Mtume s.a.w anateremshiwa wahy na kulingania Uislam Umar alikuwa ni adui mkubwa wa Uislam na Mtume (s.a.w). Kuslimu kwa Omar bin Khattab (r.a) Omar aliiƱgia ktk Uislam mwaka wa sita baada ya Utume.Mwaka huo viongozi wa Kikureish walieka mkutano wa kutafuta mtu atakayejitolea kumuua Mtume s.a.w .Omar alisimama na kusema yeye ni mtu sahihi wa kufanya kazi hiyo. Wakati yuko njiani akiwa na panga alikutana na Sa'ad bin Abii Waqas .Omar alimwambia Sa'ad "nakwenda kumuu Mtume s.a.w .Baada ya majadiliano Sa'ad alisema " Kwanza unapaswa kushuhilikia fami