Posts

Showing posts from May 27, 2019

Fursa ya ajira kwa walimu wa kiswahili huko Afrika ya Kusini

Image
Serikali za Tanzania na Kenya zachangamkia fursa ya kupeleka walimu kufundisha Kiswahili Afrika Kusini Sambaza habari hii Facebook   Sambaza habari hii Messenger   Sambaza habari hii Twitter Sambaza habari hii Ema Haki miliki ya picha IKULU, TANZANIA Image caption Rais John Magufuli na Cyril Ramaphosa wameazimia kudumisha uhusiano wa Tanzania na Afrika Kusini Rais wa Tanzania John Magufuli na mwenzake wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa wameafikiana kuhusu kufundisha lugha yaKiswahili, ikiwa ni siku chache toka mawaziri wa Kenya na Afrika Kusini kusaini makaubaliano kuhusu suala hilo. Rais Magufuli alikutana na Ramaphosa Ikulu ya Pretoria Jumapili, Mei 27 2019, ikiwa ni siku moja tu toka Ramaphosa alipoapishwa kuendelea kuliongoza taifa la Afrika Kusini. Katika mkutano huo faragha, Magufuli alimpatia zawadi ya vitabu vya Kiswahili mwenyeji wake pamoja na kamusi ya kiswahili. Afrika Kusini iliidhinisha lugha ya Kiswahili kufundishwa  katika shule za nchi hiyo Se

Alli Kiba kuendelea kuichezea Coastal

Image
UONGOZI wa Coastal Union umesema kuwa kuelekea msimu ujao hawana mpango wa kumuacha mchezaji wao Ali Kiba kwa kuwa wameridhika na uwezo wake licha ya kubanwa na majukumu yake. Kiba ambaye alisajiliwa msimu huu na Coastal Union alicheza mchezo mmoja kwenye ligi dhidi ya Mbeya City huku ule dhidi ya Kagera Sugar akifanyiwa mabadiliko dakika za lala salama. Akizungumza na SpotiXtra, Kocha Mkuu wa Caostal Union, Juma Mgunda alisema kuwa malengo yao makubwa ilikuwa ni kuunda kikosi kitakachokuwa na muunganiko mzuri msimu ujao hivyo hawana hesabu za kuwaacha wachezaji wake tegemeo. “Wachezaji wetu ambao tumeanza nao baada ya kupanda daraja ni lazima tubaki nao kwani wengi tumeanza nao mbali, hata huyu Ali Kiba nina imani tutakaa naye chini tena kuzungumza kwani licha ya kubanwa na ratiba bado amekuwa na mchango kwenye kikosi. “Mwalimu mzuri anawajua wachezaji sasa Kiba siwezi kumuacha msimu ujao jina lake lazima niwe nalo kwa kuwa kwa sasa tuna uhakika wa kubaki ligi kuu tuna

Joseph Temba awa bilionea wa kushitukiza Tanzania

Image
Joseph Temba atajirika baada ya kupata almasi kubwa zaidi Tanzania 26 Mei 2019 Sambaza habari hii Facebook   Sambaza habari hii Messenger Sambaza habari hii Twitter Sambaza habari hi Haki miliki ya picha WIZARA YA MADINI TANZANIA Image caption Mchimbaji Mdogo wa Madini Mkoani Shinyanga ameuza Almasi yake kwa Tsh. Bilioni 3. Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo ashuhudia. Taifa la Tanzania limejipatia bilionea wake wa hivi karibuni baada ya mchimbaji mdogo wa madini mkoani Shinyanga kuuza almasi yake kwa takriban dola milioni moja nukta nne sawa na Tsh. Bilioni 3. Almasi hiyo yenye karati 512 ilipatikana na mchimbaji madini mdogo Joseph Temba wiki mbili zilizopita katika eneo la Maganzo huko Shinyanga. Bwana Temba ameishukuru Wizara ya Madini na Tume ya Madini kwa muongozo na usimamizi wa Almasi yake na muongozo wa utaratibu wa mauzo ambao uko wazi. Ametoa wito kwa wachimbaji wadogo wezake kufuata utaratibu uliowekwa na Serikali kwani kuna faida nyingi hi