Posts

Showing posts from June 18, 2019

RAISI WA UTURUKI ERDOGAN ASHIRIKI SALA YA GHAIB YA JENEZA KIFO CHA RAISI WA ZAMAN WA MISRI WA CHAMA CHA MUSLIM BROTHERHOOD

Image
Rais  Erdoğan ashiriki sala ya jeneza, kifo cha Mohamed Morsi Rais wa Uturuki  ashiriki   sala ya jeneza ya kifo cha rais wa zamani wa Misri Mohamed Morsi 18.06.2019 ~ 19.06.2019 Rais  Erdoğan akemea ukimya wa  ulimwengu wa Magharibi  kwa kufumbia macho   kupinduliwa kwa rais Morsi na kuzuiliwa kwake huku  haki zake za msingi zikidhulumiwa  hadi  kupelekea kifo chake. Hayo rais wa Uturuki ameyazungumza hayo katika mkutano wa hadhara   mbelel ya hospitali ya Sultangazi Haseki mjini Istanbul. Kwa mara nyingine  rais wa Uturuki ametoa salamu za rambi rambi kwa raia wa Misri kwa kumpoteza kiongozi shujaa. Sala ya jeneza imefanyika mjini Istanbul, Yerusalemu na maeneo mengine ulimwenguni. Mjini Ankara, mkurugenzi wa idara ya masuala ya kidini Uturuki Ali Erbaş ameongoza sala ya jeneza katika mskiti wa Hacı Bayram Veli. Viongozi tofauti wameshiriki katika sala hiyo akiwemo  waziri wa sheria .

NAMNA MORSI ALIVYOFARIKI MAHAKAMANI

Image
Mohammed Morsi: Azikwa saa chache baada ya kifo,mazishi yake yahudhuriwa na familia Sambaza habari hii Facebook   Sambaza habari hii Messenger   Sambaza habari hii Twitter   Sambaza habari hii Ema Haki miliki ya picha EPA Rais wa zamani wa Misri, Mohamed Morsi amezikwa saa chache baada ya kufariki dunia akiwa mahakamani siku ya Jumatatu. Wakili wake ameliambia shirika la habari la Ufaransa, AFP kiongozi huyo wa zamani alizikwa Mashariki mwa jiji la Cairo asubuhi ya Jumanne familia yake ikiwepo Morsi,aliyekuwa na miaka 67, alikuwa kizuizini tangu alipoondolewa madarakani mwaka 2013. Makundi ya watetezi wa haki za binaadamu , ambayo yalikosoa mazingira ambayo Morsi aliwekwa,wametoa wito wa kufanyika uchunguzi kuhusu kifo chake. Familia yake na wanaharakati wamezungumzia kufo chake na muda ambao aliwekwa katika seli ya peke yake, akizuiwa kutembelewa na wanasheria na familia yake. Mtoto wake, Abdullah Mohamed Morsi, ameliambia shirika la habari la Uingereza

MORSI AAGA DUNIA MAHAKAMANI

Image
Rais wa zamani Misri Mohammed Morsi aaga dunia ghafla mahakamani Sambaza habari hii Facebook   Sambaza habari hii Messenger   Sambaza habari hii Twitter   Sambaza habari hii Email   Haki miliki ya picha GETTY IMAGES Aliyekuwa rais wa Misri, Mohammed Morsi, aliyeng'olewa madarakani na jeshi mnamo 2013 ameaga dunia ghafla akiwa mahakamani, televisheni ya taifa hilo imetangaza. Mahakama nchini Misri ilibatilisha hukumu ya kifo mnamo 2016 dhidi ya rais huyo aliyepinduliwa. Morsi alikumiwa kifo baada ya kulaumiwa kuhusika na kutoroka kwa wafungwa wengi wakati wa mapinduzi ya mwaka 2011 nchini humo. Alichaguliwa kuwa rais mwaka 2012 lakini akaondolewa katika mapinduzi ya jeshi mwaka mmoja baadaye, kufuatia maandamano makubwa ya kupinga utawala wake. Morsi alishahukumiwa kifungo cha maisha jela kwa mashtaka yanayohusu ugaidi. Umauti umemkuta alipokuwa mahakamani akisikiliza mashtaka dhidi yake ya kujihusisha kijasusi na kundi la kiislamu la Hamas la nchini

TANZANIA YAONGOZA KWA AMANI AFRIKA MASHARIKI

Image
Ripoti: Tanzania yaongoza kwa amani Afrika Mashariki Sambaza habari hii Facebook   Sambaza habari hii Messenger   Sambaza habari hii Twitter   Sambaza habari hii Email   Haki miliki ya picha IKULU TANZANIA Tanzania imeongoza Afrika Mashariki kwa mujibu wa ripoti ya Global Peace Index (GPI) inayotolewa na taasisi ya uchumi na amani (IEP)yenye makao yake makuu mjini Sydney nchini Australia. Tanzania imeshika nafasi ya 7 kwa kuwa nchi yenye amani kwa nchi za kusini mwa jangwa la Sahara na duniani ikiwa imeshuka kutoka nafasi ya 51 mwaka 2018 hadi nafasi ya 54 mwaka 2019 kati ya nchi 163, huku Iceland, New Zealand, Uholanzi, Austria, Denmark, Canada, Singapore, Slovenia, Japan, na Jamuhuri ya Czech ni nchi zilizoorodheshwa kuwa na amani zaidi duniani. Wakati Tanzania ikiongoza Afrika Mashariki, Rwanda imeifuata ikiwa ya pili Afrika Mashariki lakini imeshika nafasi ya 17 kwa nchi za kusini mwa Jangwa la Sahara, ikifuatiwa na Uganda iliyoshika nafasi ya 23 , Kenya