MAARIFA


Picha hii ilipigwa mwaka 2013 katika mbuga ya wanyama ya Maasai Mara, nchini Kenya na mpiga picha za wanyama (wildlife photographer) Alison Buttigieg, na ilishinda kuwa picha bora ya mwaka katika tuzo za habari huko Australia.
Swala huyu anayesulubiwa na chui hawa, ni Mama wa watoto wawili. Akiwa na wanae kwenye maskani yao, walivamiwa na chui waliokuwa na njaa. Watoto wake walikuwa wadogo na hawakua na nguvu za kuweza kukimbia na kujiokoa. Mama yao angaweza kuaamua kukimbia na kuwaacha wanae ambao wangeweza kuwa chakula cha chui.
Lakini hakuwaacha alikimbia nao. Baada ya umbali kidogo akaona chui wamemkaribia. Akaacha wanae waende na yeye akapunguza mwendo. Alitaka kuhakikisha wanae wanakuwa salama hata kama yeye atadhurika. Chui wakamfikia na kumparamia.
Katikati ya chui wawili bado aliweza kusimama wima na kuwatazama wanae ambao walikuwa wakizidi kuyoyoma porini. Alikuwa akiwatazama kwa mara ya mwisho maana alijua hatawaona tena!!! Ilikuwa ishara ya kuwaaga.
Kwa macho yenye ujasiri aliwaaga wanae. Aliwakodolea macho hadi wakapotelea kabisa porini kabla ya kukubali chui kumgeuza chakula. Alihakikisha kitu cha mwisho kuona kwenye macho yake ni taswira ya wanae. Ilikuwa ni ishara ya kuwaaga. Alijua hatawaona tena, lakini hakusikitika maana alijua kifo chake kilikua ukombozi kwa wanae.
Picha hii inatuonyesha taswira halisi ya Upendo wa Mama.

Comments

Popular posts from this blog

FAIDA ZA KUOA MKE ALIEKUZIDI UMRI

HISTORIA YA KHALIFA WA PILI SAYYIDNA OMAR (R.A)

Elimu kwa wanawake