NANI MUOVU ZAIDI KATI YA MUACHA SWALA NA MZINIFU?

.
NI YUPI ANA HATARI ZAIDI MBELE YA ALLAH, MZINIFU AU MUACHA SWALA?!
أَنَّ أَبَا ذَرٍّ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ حَدَّثَهُ، قَالَ : أَتَيْتُ النَّبِيَّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ وَعَلَيْهِ ثَوْبٌ أَبْيَضُ، وَهُوَ نَائِمٌ، ثُمَّ أَتَيْتُهُ وَقَدِ اسْتَيْقَظَ، فَقَالَ : " مَا مِنْ عَبْدٍ قَالَ : لَا إِلَهَ إِلَّا اللَّهُ. ثُمَّ مَاتَ عَلَى ذَلِكَ، إِلَّا دَخَلَ الْجَنَّةَ ". قُلْتُ : وَإِنْ زَنَى وَإِنْ سَرَقَ ؟ قَالَ : " وَإِنْ زَنَى وَإِنْ سَرَقَ ". قُلْتُ : وَإِنْ زَنَى وَإِنْ سَرَقَ ؟ قَالَ : " وَإِنْ زَنَى وَإِنْ سَرَقَ ". قُلْتُ : وَإِنْ زَنَى وَإِنْ سَرَقَ ؟ قَالَ : " وَإِنْ زَنَى وَإِنْ سَرَقَ عَلَى رَغْمِ أَنْفِ أَبِي ذَرٍّ ". وَكَانَ أَبُو ذَرٍّ إِذَا حَدَّثَ بِهَذَا قَالَ : وَإِنْ رَغِمَ أَنْفُ أَبِي ذَرٍّ.
(متفق عليه)
Abuu Dharr amehadithia kuwa 'Nilimwendea mtume wa Allaah nikakuta amevaa nguo nyeupe mno hali ya kuwa amelala (Nikamwacha) Kisha nikamwendea tena hali kashaamka akasema
*"Mja yeyote atayesema
لا إله الا الله
(hapana isipokuwa Allah yaani anatamka neno hili katika ulimi na kuitakidi moyoni kisha akawa amejiweka mbali na yale yote yenye kutengua neno hili kama vile shirki na mengineyo)
Kisha akafa ktk hilo ataingia peponi*" Nikasema (Abuu Dharr): Hata kama akizini na kuiba?" Akasema *Hata kama akizini na kuiba*". Nikasema tena: Hata kama akizini na kuiba? Akasema *"Hata kama akizini na kuiba*" Nikasema kwa mara nyingine "Hata kama akizini na kuiba? Akasema *"Hata kama akizini na kuiba na juu ya kulichukia hilo Abuu Dharr*" Na Abuu Dharr alikuwa akihadithia hadithi hii (Kwa wengine) husema "Na hata kama atalichukia hilo Abuu Dharr"
(Bukhari na Muslim)
Katika ITIKADI ya Ahlis Sunnati Waljamaa, mzinifu ni mwislamu, mlevi ni mwislamu, mwizi ni mwislamu na Wengineo wengi. Kwa kuwa hakuna andiko lolote kutoka katika Qur'an wa Sunna linalo tuthibitishia kuwa hao walio tajwa hapo juu ni makafiri. Andiko hilo hakuna. Isipokuwa wao ni waasi wanamuaswi Allah. Ni sawa sawa Allah atawaadhibu kwa kuwa tupa motoni lakini bado ni waislamu watatole na kuingizwa katika Pepo muda ambao wataku wanaitakidi neno hili. Na wala asithubutu mtu kufungua mlango wa zinaa kwa kisingizio cha hadith hii. Hadith hii hairuhusu zinaa bali inakataza zinaa.
Huyu ni mzinifu vipi muacha swala?
Hii hapa hadith:
" بين الرجل وبين الكفرو الشرك ترك الصلاة".
"Kati ya mtu na kati ya ukafiri na shirki ni kuacha swala".
Yaani kinacho mtenganisha mwislamu na ukafiri na shirki ni swala. Akiiacha anauingia ukafiri na shirki nao ukafiri na ushirikina unamuingia.
خرجه الإمام مسلم في صحيحه ، عن جابربن عبدالله رضي الله تعالى عنهما- عن النبي - صلى الله عليه وسلم
Hadith hii ameitoa Imaam Muslim katika Swahihi yake kutoka swahaba Jaabiri bin Abdillaah Allah amridhie kutoka kwa Mtume
صلى الله عليه وسلم.
Amesema Imaam Bin Baaz rahimahu Allah kuwa ulamaa wanasema:
"والكفر إذا عرف فهو كفر أكبر، وهكذا الشرك إذا عرف فهو شرك أكبر،
Ukafiri ukiwa ni maarifa yaani kwa Alif na laam hivi
" الكفر"
yaani kwa kiambisho au kiarifisho fasaha (definite article) " The", basi ni ukafiri mkubwa na shirki ni hivyo hivyo inapo tajwa kwa maarifa basi ni shirki kubwa,
فالمعنى بين الرجل وبين الوقوع في الكفر الأكبروالشرك الأكبر تركه الصلاة،
Hivyo maana yake ni hivi: kati ya mtu na kati ya kutumbukia katika ukafiri mkumbwa na kutumbukia katika ushirikina mkubwa ni kuacha kwake (mtu huyo) swala".
Na yafahamika kuwa mshirikina au kafiri hana makazi mbele ya Allah zaidi ya moto kwa majina yake yote. Ebu acha uvivu ndugu yangu.
Kwani ni gharama gani ilio kushinda mpaka ikapelekea ushindwe swala?!
الله المستعان

Comments

Popular posts from this blog

FAIDA ZA KUOA MKE ALIEKUZIDI UMRI

HISTORIA YA KHALIFA WA PILI SAYYIDNA OMAR (R.A)

Elimu kwa wanawake