Posts

Showing posts from June 16, 2019

AFYA

Image
Ummy Mwalimu: Tanzania Kenya, zazindua mpango wa ukaguzi wa Ebola mipakani Sambaza habari hii Facebook   Sambaza habari hii Messenger   Sambaza habari hii Twitter   Sambaza habari hii Email   Haki miliki ya picha @UMWALIMU WaTanzania wameombwa "wasiwe na hofu" kuhusu kusambaa kwa Ebola, waziri wa afya Ummy Mwalimu amesema kufuatia taarifa za Ebola kuingia Uganda kutoka Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo. Mpaka wa Tanzania unashikana na wa Congo, ambako virusi vya ugonjwa huo vimesababisha vifo vya takriban watu 1, 400. Kauli hii inatolewa wakati Uganda imethibitisha kwamba kuna visa visaba vya watu wanaoshukiwa kuugua ugonjwa huo nchini Katika ujumbe kwenye mtandao wa Twitter, Bi Mwalimu amesema Tanzania "imekuwa ikichukua hatua za utayari wa kukabiliana na ugonjwa huu" Hakimiliki ya Picha @umwalimu @UMWALIMU Hapo jana Tanzania, pamoja na Kenya, zilizindua mpango wa ukaguzi wa watu wanapovuka mipaka kuingia katika nchi hizo. Mpango h

KUMBUKUMBU:

Image
Leo Juni 16 ni siku ya Mtoto wa Afrika. Historia ya siku hii ilianza mwaka 1991 baada ya Umoja wa Afrika kuamua kuitangaza siku hii kwa ajili ya kuenzi watoto wa mji wa Soweto nchini Afrika Kusini waliouawa na askari wa Kikaburu mwaka 1976, waliokuwa wakiandamana wakipinga vitendo vya unyanyasaji na ubaguzi wa rangi uliokuwa ukiendelea, na pia kuhamasisha dunia kupinga vitendo vya kikatili kwa watoto. Askari hao waliwafyatulia risasi na kuua watoto zaidi ya 170 na kuj eruhi mamia wengine. Tukio hili lilishtua dunia nzima na mpaka sasa limebaki kama kielelezo cha matukio mabaya yaliyotakana na ubaguzi wa rangi barani Afrika. Pichani ni mtoto Hector Pieterson (13) ambaye ni miongoni mwa watoto waliouawa na askari wa Kikaburu, akiwa amebebwa na mwanafunzi mwenzake Mbuyisa Makhubo, pembeni akiwa na dada yake Antoinette ambaye mpaka sasa bado yuko hai. # AchaUkatiliKwaWatoto # LindaHakiZaWatoto