BIKRA ILIVYOKUA INAWATUNZA WANAMWARI ZAMANI NA ILIVYOGEUKA ADIMU LEO
Shuka jeupe: Jinsi mila za ubikira zinavyoendelea kuwazonga maharusi wa leo Sambaza habari hii Facebook Sambaza habari hii Messenger Sambaza habari hii Twitter Sambaza habar "Alipoanza kuvua nguo mbele yangu baada ya harusi, nilijawa na woga moyoni," anakumbuka Elmira (si jina lake halisi). "Japo nilijitahidi kuukubali uhalisia wa maisha ya baada ya kuolewa, haikunipoza woga wangu hata kidogo. Kichwani mwangu nikawa najiambia kuwa inanipasa nami nianze kuvua nguo." Elmira alikuwa na miaka 27 alipoolewa, alikuwa mhitimu wa Chuo Kikuu na akifanya kazi kama mkalimani. Alichaguliwa mume na wazazi wake. Alikubali kuolewa ili "kumfanya mama awe na furaha." "Alikuwa ni jirani yetu, lakini tulikuwa ni watu tofauti kabisa; yeye hakuwa na elimu, hatukuwa na kitu chochote cha kutuunganisha," anakumbuka Elmira. "Nilitambulishwa kwake na kaka zangu, na waliniambia kuwa alikuwa ni mtu mwema. Mama alijawa na furaha kuw...