Posts

Showing posts from June 1, 2019

KABILA AMBALO HUWAPA WAGENI MSICHANA WA KULALA NAE

Image
KABILA AMBALO WANAWAKE HUWAPA PENZI WAGENI KAMA ISHARA YA HESHIMA Kabila la OVAHIMBA ambalo linapatikana kaskazini mwa Namibia katika mikoa ya Kunene na Omusati, bado wana utamaduni wa kuwapokea au kuwakaribisha wageni wa kiume kwa kufanya mapenzi wakiamini kuwa hiyo ndiyo heshima anayostahili mgeni. Kwa mujibu wa mila zao, mgeni anapowasili kwa siku ya kwanza kama ilivyo kawaida huandaliwa chumba na kisha hupewa mwanamke/binti ambaye hajaolewa kwenye familia kulala na mgeni  kitanda kimoja kwa siku ya kwanza. Na kama kwenye familia aliyofikia mgeni hakuna mwanamke ambaye hajaolewa basi wanaume wa familia hiyo hupiga kura ili mmoja wao kumuachia mgeni chumba chake alale na mkewe. Iwapo mwanaume huyo nyumba yake itakuwa na chumba kimoja na sebule basi atamuachia mkewe alale na mgeni chumbani kwake. Kwa maelezo ya makala iliyochapishwa na mtandao wa Shirika la Habari la AP, imeelezwa kuwa wanawake huwa hawana njia ya kukataa maamuzi hivyo moja kwa moja hutii maamuzi ya wana

Mwanamke mmoja ajipasua tumbo kumtoa mtoto

Image
Mwanamke mjamzito ajifanyia upasuaji na kutoa mtoto Tanzania Sambaza habari hii   Sambaza habari hii Messenger   Sambaza habari hii Twitter   Sambaza habari hii Email   Haki miliki ya picha GETTY IMAGES Mwanamke mmoja anadaiwa kujipasua tumbo kwa kitu chenye ncha kali na kumtoa mtoto, wilayani Nkasi mkoani Rukwa Kusini Magharibi mwa Tanzania. Tukio hilo limevuta hisia za wengi na wengine wakiwa katika taharuki wengi wakifika katika kituo cha afya kushuhudia ukweli wa tukio hilo linalodaiwa kutekelezwa na bi Joyce Kalinda. Wakati taarifa za awali zikisema kuwa mwanamke huyo alijipasua umbo, Mganga mkuu wa wiaya ya Nkasi Dokta Hashi Mvogogo alizungumza na gazeti la Habari Leo alisema bado uchunguzi unafanyika ili kujua ukweli wa kilichotokea kwa mama huyo. Uchunguzi unafanyika kubaini kama alijifanyia upasuaj mwenyewe kutoa mtoto au kuna mtu mwingine alifanya hivyo. Daktari huyo amesema saa tisa alfajiri ya kuamkia siku ya Alhamisi, mwanamke huyo alifika kat

AFYA

Image
MAGONJWA MAPYA YA ZINAA AMBAYO NI TISHIO; 1: NEISSERIA MENINGITIDES Neisseria meningitidis pia hufahamika kama meningococcus, husababisha uvimbe hatari wa tando za uti wa mgongo na ubongo. Bakteria huyu amekuwa akipata umaarufu zaidi kwa kusababisha maambukizi kwenye maungo ya uzazi. 2: SHIGELLA FLEXNERI higella flexneri husababisha maumivu makali ya tumbo na kuhara damu ambapo hustawisha kusambaa kwa bakteria hao. Shigellosis husababishwa kwa kugusa moja kwa moja au kwa njia moja au nyengine kinyesi cha binadamu. 3: LYMPHOGRANULOMA VENEREUM (LGV) LGV, mwanzo hutokea kama kipele au lengelenge kisha kushambulia mfumo wa kinga ya mwili na hivyo kusababisha uwezekano mkubwa wa kupata maambukizi ya virusi vya Ukimwi. Ugonjwa huu pia husababisha maambukizi katika njia ya haja kubwa na pia kusababisha maumivu makali ya tumbo. 4: MYCOPLASMA GENITALIUM Mycoplasma genitalium ni hatari sana kwa mfumo wa uzazi kwa wanawake. Maambukizi ya Mycoplasma genitalium ambayo kwa kawaida hayana d

TEKNOLOJIA

Image
TEKNOLOJIA: Mkurugenzi wa Taasisi ya Twaweza ashiriki mkutano wa Kimataifa kwa njia ya video > Aidan Eyakuze akiwa nchini Tanzania aliweza kushiriki na kutoa maoni yake katika mkutano wa Uendeshwaji wa Serikali kwa Uwazi uliofanyika nchini Canada > Eyakuze hakuweza kusafiri kuhudhuria mkutano huo kutokana na hati yake ya kusafiria kushikiliwa na Idara ya Uhamiaji #MYD Technology

Mzee wa Sumbawanga aeleza anavyotengeneza radi

Image
MZEE WA SUMBAWANGA AELEZA ANAVYOTENGENEZA RADI Mzee Fabiani mwenye umri wa zaidi ya miaka 80 anayeishi Sumbawanga mkoani Rukwa ambaye ni maarufu sana kutokana na uwezo wake wa kutengeneza radi kwaajili ya kujikinga na mabaya pamoja na kutoa tiba mbalimbali za asili kwa watu wenye magonjwa au matatizo yao mengine amefunguka jinsi anavyotengeneza radi na kuituma. Mzee Fabiani amefunguka jinsi anavyotoa huduma zake kwa watu mbalimbali ikiwemo watu wa kutoka mataifa tofauti kama Congo, Kenya na hata Afrika Kusini ambao mara nyingi wamekuwa wakienda mpaka Sumbawanga kutafuta tiba yake hiyo. Mzee Fabiani amesema ni kweli ana uwezo wa kutengeneza radi na kuituma kwa mtu au sehemu yoyote ile ambapo kuna mbaya wa mtu na kupelekea madhara kwa mtu huyo hata kama ni mchana kweupe pasipo na mvua. Mzee Fabiani amesema kuwa ila hupenda kutuma radi hiyo Vipindi au nyakati za mvua ili kuepuka taharuki na mtafaruku katika jamii ambapo huona kuwa ni kawaida radi kupiga wakati

Pastor Awatukana Maaskofu ,atishia kufunga Kanisa

Image
PASTOR ATUKANA MAASKOFU, ATISHIA KUFUNGA KANISA +9 Mchungaji awatukana Maaskofu, ‘Wajinga sana nyie’ Mchungaji maarufu nchini Kenya, James Maina Ng’ang’a wa Kanisa la Neno Evangelist Ministry ametishia kufunga  matawi ya kanisa lake la Neno Evangelism kwa madai kuwa Maaskofu hawamheshimu mke wake. Katika kanda ya video iliyosambaa katika vyombo vya habari, ameonekana akiwakaripia maaskofu kwamba atawafukuza wote iwapo hawataheshimu onyo lake akidai kuwa matawi hayo yamekuwa vibanda na sio makanisa. ”Wakati huu nitawaonyesha uwezo wangu, mwanamke yeyote ambaye hatamuheshimu mke wangu, mlinikuta hapa na wake zenu, mmejitajirisha kupitia juhudi zangu, Wajinga nyie, Wajeuri, Takataka nilikuwa nikihubiri katika mikokoteni mpaka hapa nilipofikia, naapa mbele ya Mungu nitawaonyesha Ng’ang’a ni nani,”amesema Ng’ang’a Aidha, amewaonya kwamba kama hawatamheshimu yeye na mke wake atawafukuza katika kanisa lake bila kujari vyeo walivyo navyo hivyo wanatak