Posts

Showing posts from June 3, 2019

TAARIFA YA SERIKALI KUHUSU MJAMZITO ALIEJIPASUA

Image
TAARIFA YA SERIALI KUHUSU MJAMZITO ALIYEPASUA TUMBO LAKE NA KUTOA MTOTO Kuanzia Mei 30, 2019 kuna taarifa zilizosambaa na kutolewa na baadhi ya vyombo vya habari na mitandao ya kijamii kuhusu mama mjamzito anayesemekana kujijeruhi maeneo ya tumboni na kupelekea kutoa mtoto tumboni, tukio lililotokea katika kata ya Kirando Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi Mkoani Rukwa. Baada ya kupokea taarifa hizo timu ya ufuatiliaji iliyoundwa na wataalam wa Afya kutoka ngazi ya Mkoa na Wilaya husika ikiongozwa na Mganga Mkuu wa Mkoa ilifanya ufuatiliaji wa tukio hilo kwa lengo la kupata uhalisia wake na kubaini mambo yafuatayo: 1. Mhusika katika tukio hili ni Bi Joyce Mweupe Kalinda mwenye umri wa miaka 32 anayeishi katika Kitongoji cha Kalya, Kijiji cha Kamwanda, Kata ya Kirando, Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi Mkoa wa Rukwa, umbali wa takribani kilometa moja kutoka Kituo cha Afya Kirando. 2.Bi Joyce alipokelewa katika kituo cha Afya Kirando kilichopo katika kata ya kirando Halmashauri ya W

TIMU ITAKAYOGOMEA MECHI KURUSHWA LIVE ITAHESABIKA HAIKUFIKA UWANJANI=TFF

Image
TFF YAIONYA PAMBA"TIMU ITAKAYOGOMEA MECHI KURUSHWA LIVE ITAHESABIKA HAIKUFIKA UWANJANI" Mechi za play off kati ya Pamba SC vs Kagera Sugar FC, na Geita Gold FC vs Mwadui FC zilizokuwa zichezwe (Juni 2) zimesogezwa mbele hadi ( Juni 3 ) kutokana na sababu za kiusalama. Taarifa hiyo imetolewa na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) ikieleza kuwa usalama wa magari ya Azam TV ulikuwa mdogo kutokana na baadhi ya mashabiki kutishia kuvunja vioo wakipinga mechi hizo kuoneshwa moja kwa moja. Kwa mujibu wa TFF, mechi hizo zote zikiwemo za marudiano zitakazochezwa Juni 8, 2019 zitaoneshwa moja kwa moja ( live ) na kituo cha Televisheni cha Azam TV. “Kwa mujibu wa kanuni za ligi, haki za matangazo ya televisheni ni mali ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF). Timu itakayozuia mechi yake kuoneshwa, itahesabika kuwa haikufika uwanjani, hivyo itachukuliwa hatua kwa mujibu wa kanuni,” imeeleza sehemu ya taarifa hiyo ya TFF. Aidha TFF imewataka viongozi wa timu husika kuep

Alietelekezwa na mumewe baada ya kujifungua mapacha wanne achangiwa mlioni 32 na Wabunge

Image
Radhia Solomon, mkazi wa Mtaa wa Chemchemi, Magomeni Mapipa jijini Dar es Salaam aliyejifungua watoto mapacha wanne na kutelekezwa na mume wake amechangiwa na wabunge wote waliopo bungeni Sh. Milioni 32,050,000. Wabunge wanawake watakatwa Sh50,000 na wanaume Sh100,000 kwa ajili ya kumsaidia Radhia Solomon (24) mkazi wa Kinondoni aliyejifungua watoto wanne Januari 8, 2019. Radhia ametembelea bungeni jijini Dodoma leo Jumatatu Juni 3, 2019 na baada ya kutambulishwa na Spika Job Ndugai, alipendekeza wabunge kutoa kiasi cha fedha zao za posho leo kwa ajili ya kumchangia mwanamke huyo ombi lililokubaliwa na wawakilishi hao wa wananchi baada ya kutelekezwa na Mume wake Kati ya fedha hizo wabunge wakiume 248 kila mmoja amechanga Sh.100,000 na wabunge wa kike 145 wamechanga Sh.50,000. TOA MAONI YAKO KISHA  # SHARE

KAZI YA BODIGADI WANGU NI KUANGALIA NACHOKULA,GARI NK.PESA IKIWEPO ITUMIE!LULU DIVA

Image
Lulu alifunguka kuhusu majukumu ya bodigadi wake huyo aliyemtaja kwa jina la Beatrice kuwa ni kuangalia anakula nini, kumchagulia nguo za kuvaa kwenye shoo, kumbebea pochi na kukagua gari lake kabla hajapanda kwa kile alichosema, “ya walimwengu ni mengi”. “Si unajua ya walimwengu ni mengi sana, lazima kabla sijapanda kwenye gari anikagulie na kuangalia kama pako salama, pesa ikiwepo ni kuitumia ipasavyo,” alisema Lulu Diva kwa tambo. Aidha, Lulu alitaja mshahara anaomlipa bod igadi huyo kuwa ni shilingi milioni moja kila mwezi ambapo ameridhia mwenyewe na wanaelewana kwa kiwango hicho. “Unajua niliamua kumchukua bodigadi wa kike kwa sababu ndio tunaelewana, anaweza kuelewa lugha ninayoongea tofauti na wengine wa kiume kunielewa ingekuwa ngumu,” alisema Lulu. Lulu ni msanii wa muziki aliyeanzia kwenye filamu, baadaye akaingia kwenye kupamba video za wasanii ‘video queen’ kisha akatoboa na kuingia kwenye muziki wa Bongo Fleva ambapo mpaka sasa ameshatoa nyimbo nyingi zinazoba