KIPAJI

MUNGU HAMTUPI MJA WAKE: Licha ya ulemavu alionao mtoto Anzilan Mayani mkazi wa Ilolo wilayani Mbozi mkoani Songwe, amekuwa akishangaza watu wengi kutokana na kipaji alichonacho ukizingatia hajawahi kupata elimu yoyote.
Anzilan ni binti mwenye umri wa miaka 14, licha ya kuwa na ulemavu huo ambao umepelekea kutojiweza kwa lolote bado Mwenyezi Mungu amempa kipaji cha kuchora kwa kutumia miguu bila kufundishwa na mtu yeyote bali kwa kupitia picha anazoziona kwenye magazeti ama kwa kumuangalia mtu.
Kutokana na kutoweza kufanya jambo lolote, imekuwa vigumu kwake kupata fursa ya masomo kutokana na kukosa watu wa kumuhudumia na hivyo kuishia kukaa nyumbani tu.

Comments

Popular posts from this blog

FAIDA ZA KUOA MKE ALIEKUZIDI UMRI

HISTORIA YA KHALIFA WA PILI SAYYIDNA OMAR (R.A)

Elimu kwa wanawake