Posts

Showing posts from May 31, 2019

Wafahamu Malaika na kazi zao

Image
WAFAHAMU MALAIKA NA KAZI ZAO. 👉 JIBRIIL Huyu ni Malaika mkubwa kabisaa kati ya Malaika wote aliyowaumba ALLAH (S.W.), Malaika huyu ana mbawa takribani 600. Kazi  kubwa ya Malaika huyu ni kuteremsha Wahyi (ufunuo) kwa Mitume, tokea kwa Adamu (A.S.) mpaka Mtume wa mwisho Muhammad (S.A.W). 👉  MALAKUL MAUTI Huyu ni Malaika maarufu sana kufahamika kwa watu wengi. Malaika huyu amepewa jukumu na ALLAH (S.W.) la kutoa Roho (Nafsi) za watu. Malaika huyu kapewa uwezo wa kuingia popote pale ili kutoa Roho ya mtu ambaye muda wake umeshafika wa kuondoka hapa duniani, hata kama mtu huyo awe na ulinzi kiasi gani. ALLAH amemtaja Malaika huyu kwenye Qur'an pale aliposema, "Sema: Atakufisheni Malaika wa Mauti aliyewakilishwa kwenu, kisha mtarejeshwa kwa mola wenu." Surat Assajida: 11. 👉  RAQIIB NA A'TIID Hawa ni Malaika wawili mmoja anakaa upande wa kulia wa mwanadamu na mwengine anakaa upande wa kushoto wa mwanadamu. Kazi yao kubwa ni kuandika matendo (Amali) ya

ELIMU

Image
Wanasayansi watengeneza ukungu wa kijenetiki unaoteketeza 99% ya mbu wanaoeneza malaria Sambaza habari hii Facebook   Sambaza habari hii Messenger   Sambaza habari hii Twitter Sambaza habari hii Email   Haki miliki ya picha SCIENCE PHOTO LIBRARY Ukungu (fangasi) - ambao umeboreshwa kisayansi kutoa sumu ya buibui - unaweza kuua idadi kubwa ya mbu wanaoambukiza malaraia, utafiti mpya wa kisayansi umebaini. Majaribio ya ukungu huo, ambayo yamefanyika nchini Burkina Faso, Afrika Magharibi yameonesha kuwa idadi ya mbu iliteketezwa kwa 99% ndani ya siku 45. Watafiti wanasema si lengo lao kutokomeza mbu hao bali kusaidia kuzuia maambukizi ya malaria. Ugonjwa wa malaria, unaoambukizwa na mbu jike aina ya Anopheles wanyonyao damu huua zaidi ya watu 400,000 kwa mwaka. Duniani kote, wagonjwa milioni 219 wa malaria kila mwaka huripotiwa. Kwanini Saudia na Iran ni maadui wakubwa? R. Kelly akabiliwa na mashtaka mapya 11 ya unyanyasaji wa kingono Je umewahi kusikia m

AFYA

Image
Simulizi ya Lucky Ndanu, mama aliyepoteza titi kutokana na saratani Paula Odek BBC Swahili Sambaza habari hii Facebook   Sambaza habari hii Messenger   Sambaza habari hii Twitter Sambaza habari hii Email   Haki miliki ya picha LUCKY NDANU Image caption Lucky Ndanu Lucky Ndanu mwenye umri wa miaka 31 alipatwa na saratani ya matiti alipokuwa na miaka 19. Saratani yake ilikuwa katika kiwango cha kwanza . Ameishi bila titi moja kwa takribani miaka 12. Bi Ndanu alianza kuhisi shida ya matiti mwaka 2007 alipokuwa katika mwaka wake wa mwisho katika taasisi moja ya kielimu nchini Kenya Alikuwa akipata maumivu makali kila alipokuwa akivua sidiria hasa katika titi lake la upande wa kulia. Amesema titi lake la upande wa kulia lilikuwa na mishipa iliyokuwa inajaa damu kila wakati na lilikuwa na kiwango kikubwa cha joto na tofauti kabisa na titi lake jingine. Miaka iliyopita aligundua alikuwa na uvimbe lakini hakuutilia maanani kwani alifikiria ni jambo la kawaida