Posts

Showing posts from December 6, 2019

MCHUNGAJI MBARONI KWA KUWANYWESHA SUMU WAUMINI WAKE

Image
Mchungaji mbaroni kwa kuwanywesha dawa ya kujichubua waumini kwa madai kuwa inatibu magonjwa. #1 Mchungaji Sam Little (25) ambaye ni raia wa Uingereza amekamatwa nchini Uganda kwa tuhuma za kuwanywesha waumini wake dawa ya kujichubua na kuwaaminisha kuwa ni tiba ya miujiza inayotibu magonjwa ya malaria, saratani (kansa) na Ukimwi. Mchungaji huyo wa Kanisa la Global Healing Christian Missions alikamatwa hivi karibuni baada ya gazeti la Guardian la Uingereza kufi chua mtandao wa uovu huo na kuainisha namna Little alivyokuwa anashirikiana na mchungaji mwingine Robert Baldwin kutoka Marekani kusambaza dawa hiyo iliyopewa jina la ‘mchanganyiko wa madini wenye miujiza’ kwa kifupi MMS. Sam Little ambaye anatokea katika mji wa Bedfordshire nchini Uingereza, alikamatwa na askari wa Uganda katika makazi ya Kanisa lake lililopo katika kijiji cha Kitembi, maili chache kutoka mji wa Fort Portal uliopo magharibi mwa Uganda. Mbali na mchungaji huyo pia walikamatwa raia