Posts

Showing posts from December 11, 2019

Namna ya kuandika ombi la mkopo

Namna ya kuandika ombi la Mkopo Kuna dhana imejengeka miongoni mwa jamii kuwa si rahisi na kuna usumbufu mkubwa kwa wajasiriamali wadogo na wakati katika  kupata mkopo. Dhana hii sio sahihi kabisa. Itambulike kuwa mabenki yanapata pesa kupitia utoaji wa mikopo, kama yasipotoa mikopo ni dhahiri kuwa yatapata ugumu katika kujiendesha. Kudhihirisha hilo hivi karibuni mabenki mengi yametangaza kupunguza riba za kukopesha ili tu kuwavitia watu wengi zaidi waweze kukopa. Benki ya CRDB kwa mfano, imepunguza riba ya mikopo binafsi kutoka asilimia 22 hado asilimia 16 na imeongeza mda wa kulipa deni kutoka miaka minne hadi miaka saba. Benki ya NMB kwa  upand mwingine imepunguza riba hadi asilimia 17 na benki ya BOA imepunguza riba hadi asilimia 11. Hii inaonyesha ni kwa kiasi gani mabenki yanategemea biashara ya kukopesha ili yaweze kujipatia kipato. Tatizo kubwa ambalo limekuwa likifanya mabenki yasitesite kukopesha ni uelewa mdogo wa wajasiriamali katika masuala ya fedha na jinsi

Namna ya Kuandaa Mchanganuo wa biashara

Maana ya na umuhimu wa mchanganuo Mchanganuo wa biashara ni andiko ambalo linaweka bayana malengo na madhumuni ya biashara na namna yatakavyofikiwa. Ni mpangilio maalum wa kuongoza utekelezaji wa kufanikisha lengo la biashara. Kuandaa mpango wa biashara ni muhimu kwa mafanikio ya biashara yoyote. Mchanganuo wa biashara hutoa dira na kusaidia kuongoza uendeshaji wa biashara. Mara nyingi ni sharti mojawapo katika kuomba mkopo. Mpango wa biashara ulioandaliwa vizuri utatoa majibu ya maswali mbali mbali kama vile nini madhumuni ya biashara yako, Utamwuzia nani/akina nani? Ni yapi malengo yako ya mwisho? Utagharimia vipi biashara yako? na mengine mengi Mpango wako wa biashara utakusaidia kutafakari mwelekeo wa kampuni yako na namna ambavyo itakabiliana na changamoto mbalimbali ili iwe endelevu. Vipengele muhimu vya Mchanganuo wa Biashara Vipengele muhimu vya Mchanganuo wa Biashara ni kama vifuatavyo:- 1. Ufupisho Kipengele hiki huandikwa mwishoni. Andika katika kipengele hiki mambo

Jinsi ya kuandaa mpango wa biashara (Business Plan)

Image
  Thread starter Start da #1 Mpango wa Biashara  (Business Plan) , ni nyenzo muhimu katika mafanikio ya biashara. Mpango wa Biashara humsaidia mjasiriamali ku-shape wazo lake la biashara na kulifanya kuwa fursa  (Opportunity). FAIDA ZA KUWA NA MPANGO WA BIASHARA Hutoa taarifa za msingi juu ya biashara; zinazomuwezesha mjasiriamali kutafuta vyanzo vya fedha kwa ajili ya kuendeshea biashara. Huweza kutumika kwa ajili ya kuvuta rasilimali watu. Humsaidia mjasiriamali katika kutafuta na kupata mshirika/washirika katika biashara (Strategic Partiner/Suppliers) Mpango wa Biashara hupaswa kujikita katika maeneo ya msingi (critical aspects) za mfumo wako wa biashara (business model) na kutoka hapa ndipo tunapata mtindo au "format" ya Mpango wa Biashara. Busara (wisdom) ni kuamini kwamba Mpango wa Biashara ni nyaraka iishiyo  "living document"  maana ya dhana hii ni kwamba; kadiri siku zitakapokuwa zinakwenda, Mpango utakuwa unahuishw