Posts

FITINA YA MAREKANI KWA GAS YA URUSI

Image
UKISTAAJABU MAAJABU YA FITNA ZA GAS YA MTWARA UTAYAONA MAAJABU YA FITNA ZA MAREKANI KWA GAS YA URUSI Mradi wa bomba la gas asilia ya bei nafuu kutoka Urusi kupitia bahari ya baltic Finland Serbia mpaka Ujerumani uitwao Nord Stream two uko mbioni kukamilika licha ya presha kumbwa ya tishio la vikwazo na misukosuko ya vitisho vya Marekani kuziwekea vikwazo mabenki kampuni za Urusi Ujerumani Italy na Ulaya zilizohusika katika usambazaji wa mitaji vifaa nyenzo teknolojia nakadhalika . Kufanikisha mradi huo kwa Urusi ni robo ya ushindi dhidi ya kuutumia utajiri wao wa rasilimali gas kuwa si tu bidhaa bali silaha ya kulinda maslahi yao ya kiuchumi na kisiasa. Kwa wajerumani napo ni uzoefu mpya kwa kuvuka hatua ya kwanza ya kubishana na mume mbabe bila kupigwa makofi tangu walipozwa kisiasa kiuchumi na kijeshi kama malipo ya uharibifu wa vita kuu mbili za dunia alizozianzisha na kupiwa kwa uzembe mdogo tu wa kujaribu kupiga msamba kwenye maeneo yenye utelezi wa barafu za Jumuiya ya kis...

HISTORIA KWA UFUPI

Image
Msikiti Mtukufu wa Makka, huu ni msikiti mkongwe ambao kiasili kabisa ulianza kujengwa (kuwekwa msingi) na Nabii Adamu (Adamu huyu tunaemjua baba wa watoto wa Adamu na mume wa mama yetu Hawa ) na baada ya karne nyingi kupita ulikuja kujengwa upya na Nabii Ibrahimu akishirikiana na mwanae Ismail toka hapo ukaendelea kuboreshwa kadri teknolojia zinavyokua na mahitaji ya watu kuongezeka. Hii ni nyumba ya ibada inayobeba watu wengi kwa wakati mmoja kuliko nyumba za dini zote duniani kwani huingiza karibu watu milioni tatu kwa mara moja. Ibrahimu alikuwa na watoto wawili, Ismail kwa mkewe mdogo(hajra) ambae huyu Ismail kizazi chake ndio baadae alikuja kuzaliwa Nabii Muhammad Swalallah alayhi wasalama, na Is'haka kwa mke mkubwa ambae awali hakuwa akizaa mpaka akamuamuru mumewe aoe ili wapate mtoto baada ya mumewe kumuoa kijakazi wake Allah akaleta miujiza yake huyu mama Sara akashika mimba akiwa na zaidi ya miaka sabini, na hii ilikuwa baada ya Hajra (mke mdogo kupata...

MCHUNGAJI MBARONI KWA KUWANYWESHA SUMU WAUMINI WAKE

Image
Mchungaji mbaroni kwa kuwanywesha dawa ya kujichubua waumini kwa madai kuwa inatibu magonjwa. #1 Mchungaji Sam Little (25) ambaye ni raia wa Uingereza amekamatwa nchini Uganda kwa tuhuma za kuwanywesha waumini wake dawa ya kujichubua na kuwaaminisha kuwa ni tiba ya miujiza inayotibu magonjwa ya malaria, saratani (kansa) na Ukimwi. Mchungaji huyo wa Kanisa la Global Healing Christian Missions alikamatwa hivi karibuni baada ya gazeti la Guardian la Uingereza kufi chua mtandao wa uovu huo na kuainisha namna Little alivyokuwa anashirikiana na mchungaji mwingine Robert Baldwin kutoka Marekani kusambaza dawa hiyo iliyopewa jina la ‘mchanganyiko wa madini wenye miujiza’ kwa kifupi MMS. Sam Little ambaye anatokea katika mji wa Bedfordshire nchini Uingereza, alikamatwa na askari wa Uganda katika makazi ya Kanisa lake lililopo katika kijiji cha Kitembi, maili chache kutoka mji wa Fort Portal uliopo magharibi mwa Uganda. Mbali na mchungaji huyo pia walikamatwa raia...

karibu

Chanzo cha ajali ya lori kuwaka moto ni mtu mmoja alipojaribu kuiba betri

Image
LORI LA MAFUTA LAPINDUKA MOROGORO, LALIPUKA NA KUUA ZAIDI YA 100 Ínaripotiwa kuwa Idadi kubwa ya watu wanaokadiriwa kuwa zaidi ya 100 wanahofiwa kufa moto baada ya gari la mafuta lililopata ajali kuwaka moto mkoani Morogoro. Imeripotiwa kwamba Lori hilo lililokuwa limebeba mafuta lilikuwa linatokea Dar Es Salaam lilipofika eneo la Itigi Mzambarauni nje ya mji wa Morogoro muda ya saa moja asubuhi kukawa na mwendesha bodaboda akakatiza mbele ya lori hilo wakati mwenye lori anam kwepa ndipo lori hilo likaanguka upande wa kushoto mwa barabara, kisha akajitokeza mtu mmoja kuchomoa betri kwenye lori hilo, watu mbalimbali haswa wakiwemo waendesha boda boda nao wakafika eneo la tukio kwa ajili ya kuiba mafuta moto ukalipuka na wakapoteza maisha watu zaidi ya 100. Mashuhuda wa tukio hilo wameviambia vyombo vya habari kuwa lori la mafuta (petroli) lilipinduka, hivyo watu mbalimbali, wengi wao wakiwa madereva wa pikipiki wakaenda eneo la tukio na vibebeo kwa lengo la kupata kuchukua m...

NCHI KUMI KINARA WA USHIRIKINA DUNIANI

Image
UMEISIKIA HII?? HII HAPA ORODHA YA NCHI 10 ZINAZOONGOZA KWA MASUALA YA UCHAWI NA USHIRIKINA DUNIANI, TANZANIA NAYO IMETAJWA Tanzania imetajwa kuwa nchi ya 10 katika orodha ya nchi zinazoamini ktk masuala ya uchawi, ulozi, mapepo, imani za kishirikina na kila aina ya nguvu za giza duniani. Mtandao wa The Richest umetaja nchi 10 duniani mashuhuri kwa mambo ya ushirikina, Tanzania ikishika nafasi ya 10 ktk orodha hiyo. Bara la Afrika limetoa nchi 5, huku nafasi ya kwanza ikishikwa na Indonesia. Mauaji ya albino ni moja ya mambo yaliyoipa Tanzania alama za juu katika orodha hiyo. Orodha kamili ni kama ifuatavyo: 1. Indonesia 2. DRC 3. Ghana 4. Colombia 5. Uganda 6. Papua New Guinea 7. Nigeria 8. Nepal 9. Gambia 10. Tanzania Picha hii inaonyesha binti akiaguliwa sehemu za siri na mganga ili bwana wake akishiriki nae tendo asitamani mwanamke mwingine.Sidhani kama mganga alimuacha salama.

Baba yangu alisababisha nilale na mjomba wangu

KISA Cha Kusikitisha 'Baba Yangu Alisababisha Nilale na Mjomba Wangu, Kamwe Sitamsamehe' Nimeona leo nitoe siri yangu hapa ya muda mrefu ambayo imekuwa ikiniumi za sana pale tu ninapokumbuka, nakosa raha na amani inapotea. Kwa ufupi kabisa, nilizaliwa mkoani Mara wilaya ya Musoma mjini maeneo ya Nyakato, mama yangu alibeba mimba yangu akiwa darasa sita hivyo hakumaliza shule. Ilibidi akae nyumbani mpaka pale alipojifungua, kwa wakati kulikuwa hakuna sheria kali kwa wanaowapatia wanafunzi mimba wakiwa shule. Na aliyempatia hiyo mimba naye alikuwa mwanafunzi mwenzake lkn alikuwa la saba yeye alimaliza shule. Baba yake mama ambaye ni babu yangu alikuwa na uwezo mkubwa hivyo hakushindwa kutulea mimi na mama. Nikiwa na miaka 6 ndipo nilipokuja kumjua baba yangu wakati huo nae alikuwa amekuwa mtu mzima, alikuja akanisalimia akaondoka, kwao pia walikuwa vizuri kimaisha. Nikiwa na miaka 9 naanza darasa la kwanza wakati huo tulikuwa tunaingia shule tukiwa na umri mkubw...