HISTORIA KWA UFUPI



Msikiti Mtukufu wa Makka, huu ni msikiti mkongwe ambao kiasili kabisa ulianza kujengwa (kuwekwa msingi) na Nabii Adamu (Adamu huyu tunaemjua baba wa watoto wa Adamu na mume wa mama yetu Hawa ) na baada ya karne nyingi kupita ulikuja kujengwa upya na Nabii Ibrahimu akishirikiana na mwanae Ismail toka hapo ukaendelea kuboreshwa kadri teknolojia zinavyokua na mahitaji ya watu kuongezeka.
Hii ni nyumba ya ibada inayobeba watu wengi kwa wakati mmoja kuliko nyumba za dini zote duniani kwani huingiza karibu watu milioni tatu kwa mara moja.
Ibrahimu alikuwa na watoto wawili, Ismail kwa mkewe mdogo(hajra) ambae huyu Ismail kizazi chake ndio baadae alikuja kuzaliwa Nabii Muhammad Swalallah alayhi wasalama, na Is'haka kwa mke mkubwa ambae awali hakuwa akizaa mpaka akamuamuru mumewe aoe ili wapate mtoto baada ya mumewe kumuoa kijakazi wake Allah akaleta miujiza yake huyu mama Sara akashika mimba akiwa na zaidi ya miaka sabini, na hii ilikuwa baada ya Hajra (mke mdogo kupata mtoto)
Wakati mwingine dada zetu msikatae ukewenza hua unakuja na baraka zake' Sara alimzaa Is'haqa (isac) ambae kizazi chake baadae ndio kilikuja kumtoa Issa (Yesu) hivyo Issa na Muhammad wanakutana kwa babu mmoja Ibrahimu, (siku moja tutataja jina la Muhammad mpaka kwa Ibrahimu,
Pichani Sheikh.Dr (Abdul Rahman Assudeis) akitoa khutba kwenye swala ya Ijumaa hapo jana kwenye Huu msikiti namba moja kwa utukufu kwa imani ya uislam.
Msikiti wa pili ni wa Baitul lmuqaddas uliopo Palestina(Israel) unaogombewa kwa miaka mingi baina ya waislam na wanaojiita mayahudi wa israel (kwani kihistoria wale waliopo israel sasa sio wanawaisrael bali ni wazungu kutoka Ulaya na Marekani waliotokea baada ya vita ya ya pili ya dunia waliokuwa wakisali kwa imani ya uyahudi
Msikiti huu kiasi mpaka sasa upande huswaliwa na waislam na upande Mayahudi japo wakristo huona Israel ni wenzao na kujinasibisha nao lakini wao hawamuamini Yesu wala hawatumii Biblia na hawamkubali kabisa yesu wao wanavitabu vyao na vinaikashifu biblia .
Na msikiti wa Tatu na wa mwisho kwa Utukufu ni msikiti wa Madina maarufu masjidi nnabawi (msikiti wa mtume) ulipo mji wa madina alipomalizia maisha yake Muhammad Swala llahu alayhi wasalama.
Abuu Arif Hassan bin Khateeb Zubeir Mwagilloh

Comments

Popular posts from this blog

FAIDA ZA KUOA MKE ALIEKUZIDI UMRI

HISTORIA YA KHALIFA WA PILI SAYYIDNA OMAR (R.A)

Elimu kwa wanawake