FITINA YA MAREKANI KWA GAS YA URUSI

UKISTAAJABU MAAJABU YA FITNA ZA GAS YA MTWARA UTAYAONA MAAJABU YA FITNA ZA MAREKANI KWA GAS YA URUSI
Mradi wa bomba la gas asilia ya bei nafuu kutoka Urusi kupitia bahari ya baltic Finland Serbia mpaka Ujerumani uitwao Nord Stream two uko mbioni kukamilika licha ya presha kumbwa ya tishio la vikwazo na misukosuko ya vitisho vya Marekani kuziwekea vikwazo mabenki kampuni za Urusi Ujerumani Italy na Ulaya zilizohusika katika usambazaji wa mitaji vifaa nyenzo teknolojia nakadhalika . Kufanikisha mradi huo kwa Urusi ni robo ya ushindi dhidi ya kuutumia utajiri wao wa rasilimali gas kuwa si tu bidhaa bali silaha ya kulinda maslahi yao ya kiuchumi na kisiasa.
Kwa wajerumani napo ni uzoefu mpya kwa kuvuka hatua ya kwanza ya kubishana na mume mbabe bila kupigwa makofi tangu walipozwa kisiasa kiuchumi na kijeshi kama malipo ya uharibifu wa vita kuu mbili za dunia alizozianzisha na kupiwa kwa uzembe mdogo tu wa kujaribu kupiga msamba kwenye maeneo yenye utelezi wa barafu za Jumuiya ya kisovieti matokeo yake akatenguka kiuno na kushindwa kuumalizia umbali mdogo tu aliobakisha kuitawala Ulaya yote ya Magharibi na sehemu za Ulaya ya Mashariki kama hatua ya kwanza kuelekea kwenye ndoto ya Adolph Hitler kuwa mfalme wa dunia baada ya kumuoa Malkia Elizabeth wa Uingereza.
Wajerumani wameamua kupambania uchumi wao viwanda vyao na ustawi wa nyumba zao dhidi ya baridi kali ya Ulaya na mahitajj ya nishati safi ya umeme. Hivyo wameidhirishia Marekani katika lugha ya upole yenye jeuri kwa mbaali kuwa maslahi yao ya viwanda uchumi na watu wake kwa gas ya Urusi hayawezi kusombwa kwa siasa za mabavu wala ushawishi wa tishio la vikwazo vya Marekan ili wawe watumwa wa kununua gas ya Marekani ya bei ghali inayoletwa na meli katika hali ya umiminika LNG (Liquified Natural Gas) kama ambavyo Poland imeingia mtegoni kujikamua kununua gas hiyo ya Marekani kwa bei kubwa zaidi ili kulipa kile kinachoitwa ulinzi wa Marekani kwa Poland dhidi ya tishio la Urusi kupitia kuwekwa kwa majeshi ya Marekani nchipi Poland vifaru magari ya deraya ndege vita na mitambo ya ulinzi wa anga.
.
Uhalisia gas ya Urusi haina mshindani kiunafuu wa bei na uhakika wa usambazaji barani Ulaya iwapo tu siasa za Marekani na Ulaya za kujilinda na kuweka vikwazo vya gas hiyo barani Ulaya vitatolewa n washindani wa usambazaji wa gas barani Ulaya wakaachwa washindane kwa Uhuru kabisa si Marekani Australia Qatar mwenye ubavu wa kushindana na gas ya Urusi sokoni maana hawana unafuu wa gharama ya gas wala miundombinu ya usambazaji kama aliyonayo Urusi usambazaji wa kutumia mabomba yaliyolazwa mamia ya kilometa kutoka kwenye visima vyao vya gas vya maeneo ya barsfu na baridi kali katika miradi ya sakhalini Yamal na Yakutsk . Huwezi shindanisha gas inayotiririka kwenye mabomba na ile inayochujwa na kubinywa ijazwe kwenye mitungi maarufu kama LNG dhidi ya gas ya mabomba ya Urusi.
Urusi anataka kuikama Ulaya kinishati ili kutegemeza uchumi wake na kushindana na Marekani kiushawishi barani Ulaya kwa manufaa ya maslahi mapana ya kitaifa na ndio maana hata ile Turkish Stream pipelines inatekelezwa kati ya Urusi na Uturuki lengo si mabomba yale ya gas yaishie Uturuki bali Uturuki ni mlango wa mabara ya Ulaya na Asia hivyo Uturuki itakuwa njia panda ya usanbazaji wa gas ya Urusi kusambazwa kwa nchi za Ulaya na hata Arabuni kwa kukwepa njia za nchi zingine ambazo zimeonekana hazitabiriki kimsimamo dhidi ya hofu na kutumika na Marekani ikiwemo Ukraine na Poland.
Kumbuka Urusi ina isambazia Ulaya zaidi ya asilimia 30 ya gas yote barani Ulaya na mkakati wao mkuu wa sasa ni kujipenyeza zaidi kiutawala katika soko la gas na mafuta barani Ulaya huku ikitanua usambazaji wa mafuta na gas barani Asia ambako ukuaji wa viwanda miji na chumi za nchi nyingi ni mkubwa.
Lengo kuu la utanukaji huu kutoka kuacha utegemezi wa masoko kwa usambazaji wa bara la Ulaya pekee hasa Ulaya Magharibi na kuelekeza nguvu pia katika usambazaji wa masoko ya bara la Asia hasa Asia Mashariki kama ku diversify biashara na hatari ya athari za utetereka kwa biashara masoko ushawishi na kupunguza utegemezi wa Urusi kwa masoko na mitaji ya Ulaya hasa baada ya somo la athari ya utegemezi wake kufuatia vikwazo vya 2014 katika sekta mbalimbali za kiuchumi na siasa baada ys kuitwaa na kuirudisha tena Crimea nyumbani Urusi kufuatia kutolewa kama zawadi mwaka 1954 kwenda Ukraine kutoka Russia Republic enzi za USSR .
Mkakati mwengine wa Urusi ni kupunguza kama siyo kuua ushindani wowote dhidi ya nishati za Urusi kwa soko la mafuta na gas barani Ulaya hasa kutokea gas za kusafirishwa na meli LNG ilihali yake ni ya mabomba na ya bei rahisi na kumbuka namna Urusi ilivyoingilia kati mradi wa kujenga bomba la gas uliochochewa na Marekani kuelekea Ulaya uitwao NABUKa kutoka Kazakhstan kwenda Ulaya kwa kufanya fitna za kijasusi na uchumi mpaka Kazakhstan ikakubali iwe inazalisha gas yake na kuiuzia Urusi halafu Urusi ndo iwe inaisafirisha kwa mabomba yake na washirika kwenda kuuza Ulaya badala ya kuiruhusu Kazakhstan itie pua yake katika uzalishaji na usambazaji kama mshindani wa kibiashara kama alivyotaka Marekani ili kupunguza nguvu za Urusi kuhodhi soko la nishati ya gas barani Ulaya.
Hapa mlengwa wa kufanyiana fitna sokoni ni Marekani ambaye anataka kupunguza utegemezi wa Ulaya kwa gas ya Urusi ili kuua ushawishi wa Urusi barani Ulaya kupitia kuhodhi soko la gas ya bei nafuu hivyo kutumia gas kama silaha ili kulinda maslahi yake . Kumbuka Marekani ni mzalishaji wa gas mkubwa tu hasa za baharini na zinazoletwa na meli na kulindwa kwa ulazimisho wa manunuzi huku zikiwa na bei kubwa kuliko gas ya wauzaji wengine wakubwa kama Urusi Qatar na Australia .
Rejea pupa za Poland kununua gas ya Marekani kwa bei kubwa mno kutoka Marekani au meli za gas za Marekani kutia nanga Ureno na kusambaza gas Ulaya kama jaribio la kushindana na Urusi na dhihirisho la mshikamano wa Ulaya dhidi ya mshirika bwana mkubwa Marekani.
Pia Marekani inatekeleza mpango wa kuitumia Qatar inayozalisha gas kwa wingi kama plan B ya ushindani dhidi ya gas ya Urusi kufuatia ugumu wa gharama ya gas yake kupenya kwa upana barani Ulaya kwa bei nafuu ili kuangalia namna gani itafanikisha hili Qatar walikubaliana na Marekani kuanza fitna za kufanikisha mpango huo
zamani. Rasilimali zote zilikuwa tayari ila kimbembe kikaja kwenye njia rahisi nafuu na ya uhakika ya kupitisha mabomba ya gas kutoka Qatar kwenda Ulaya kupitia Uturuki. Shida haikuw Uturuki kimbembe kilikuw kabla ya kufika Uturuki inabidi upite Syria na hapo ndipo mzozo ulipoanza.
Syria mshirika mkubwa wa Urusi anawezaje kuruhusu mradi unaofadhiliwa na maadui zake upite katika ardhi yake ili ukahujumu maslahi ya rafiki na Washirika wake wakuu Urusi na Iran, Hee unashangaa kuiona Iran kwani hujui kuwa Iran nae ana gas na mafuta na ana ndoto za siku moja kusafirisha rasilimali hizo kwenda Ulaya kupitia Syria na Uturuki na kwenda Asia kupitia Pakistan China na hata India na nchi zingine.
Kutokea hapo ndipo machafuko ya Syria yaliandaliwa ili kukamilisha maslahi mengi ya Marekani na washirika wake mojawapo likiwa hili la njia ya kupitisha mabomba ya gas na mbaleni mafuta kuelekea Ulaya kupitia Uturuki.
Nadhami umeelewa ile kaulimbiu ya Assad must go ilitokana na sababu gani mojawapo. Marekani ma washirika wake wa Magharibi ambao ni E NATO Saudi arabia UAE Qatar nakadhalika walitaka kwanza kuung'oa ushawishi wa Urusi katika nchi za kiarabu na hasa nchini Syria ulioanzishwa tangu enzi za USSR dhidi ya utawala wa baba yake Bashar Al Assad aliyeitwa Hafeidh /Hafidh Al Assad ambao ndio mwiba mkuu na chanzo cha mkwamo na jeuri ya maslahi yao ya kinyonyaji na yenye shuruti ya utekelezaji; japo haimaanishi Warusi na Wachina hawana maslahi ya kinyonyaji maana unyinyaji ni hulka na asili ya msingi wa mwanadamu yoyote hasa mwenye nguvu.
Ambapo kuanzishwa kwa maandamano ya Arab Spring kama mkakati mkuu wa kwanza ulilenga kuzidhiofisha na kuzivunja vunja nchi za kiarabu kama nyenzo ya awali ya kuingilia katika unyonyaji ambapo ingepelekea kushamiri kwa udhibiti wa Marekani katika nchi hizo na hivyo kulindwa kwa maslahi ya Marekani kupitia uwekaji wa majeshi na nyenzo za kijeshi baada ya kupata pa kuingilia kupitia uchochezi wa maandamano yaliyopangwa kiweledi kupitia kuutumia udhaifu wa hali za maidha na tawala za nchi za kiarabu .
Sasa bhasi kwa kumuangusha Bashar Al Assad kwanza kungeung'oa ushawishi wa Urusi nchini Syria na katika maeneo ya karibu na bahari ya Mediterania hivyo kumpotezea mshindani wake mkuu ambaye ni Urusi maslahi mapana kwa kumpora mshirika wake muhimu na kuwadhoofisha Washirika wengine wa karibu hasa Iran.
Rejea umuhimu wa Syria kijeshi uchumi jamii siasa kuanzia matumizi ya Bandari ya Tartus kwa vikosi vya jeshi la maji la Urusi katika bahari ya Mediterania , njia za usafirishaji za kuiunganisha Urusi ya huku kwenye jamii za kiislamu huku North Caucasus Dangestan nchi za USSR ya kale ambazo zipo kwenye ushawishi na udhibiti wa Urusi kupitia mwamvuli wa Eurasia Economics Countries nk., kungeianguushia heshima Urusi kwa aibu ya kumpoteza mshirika, kungezuia misafara ya nishati silaha bidhaa na mizigo mengine ya siri kwenda kwa washirika wake wa Uarabuni hasa Irani na pia Syria ingetumika kuibana ziran kiuchumi na kupunguza kumpunguza kukua kwa ushawishi wa Irani katika jamii za kiarabu na kiislamu hasa kwa kudhibiti biashara za magendo zinazoipunguzia Iran mbinyo wa vikwazo vilivyowekwa kutokana ba mzozo wa matumizi ya nishati ya nyuklia pia ukuaji wa kijeshi wa washirika wa Iran na msaada wake kwa jamii za kishia ungedhibitiwa kuanzia usambazaji wake wa mafunzo ya kijeshi silaha taharifa za ujasusi na mitandao ya ukusanyaji wa wapambanaji kwa mgongo
wa Jihad ungebanwa.
Hivyo ingeathiri sana harakati za Hizbollah Palestine Houth Washia na washirika wa Iraq Syria wangebanwa mno hali ambayo ingeipunguzia presha Israel na Saudi Arabia na kuchochea mkakati wa kuivuruga Iran kinomanoma. Kubanwa sana kwa Iran kungepelekea kupungua kwa ushirikiano na Urusi hasa kutokana na msukumo mkubwa wa kudhibiti hali ya mambo ndani ya Iran badala ya mipango ya utanukaji wa nje ya Iran.
Sasa endapo Syria ingeanguka Marekani angepambania autumie ushawishi wake kwa Qatar wajenge bomba la gas liingie Ulaya kupitia Syria na Uturuki ili kuua ushawishi wa Urusi kiuchumi kupitia gas na pia kuzima ndoto za Iran kuja kutanua usambazaji wa gas yake barani Ulaya na zmashariki ya kati hasa kupitia Syria mpaka Uturuki rejea kusua sua kwa bomba la gas kutoka Iran kwenda Pakistan ziara ya mwanamfalme ambaye ni kiongozi mkuu kivuli wa Saudi Arabia Mohammed Bin salman na ahadi yake ya kuipatia Pakistani dola bilioni 10 endapo itakubali mashirikiano ya Pakistan na Saudi Arabia yenye lengo la kuibana na kuuindoa ushirika wa iran katika himaya za kiislamu hasa za huko Pakistanj Afghanstan na maeneo mengine ambapo Iran ana miradi kibao ya kivita dhidi ya maslahi ya Marekani na Saudi Arabia ambaopo Saudi Arabia nayo imelenga kushirikiana na Marekani kuhakikisha mafuta na gas ya iran hayafanikiwi kusambazwa barani Ulaya na Asia hasa China ili kuipunguzia nguvu za mapato ambazo ndo nyenzo kuu katika kugharamia miradi ya makombora ukuaji wa kijeshi usambazaji ushawishi na uwekezaji katika tafiti na maendeleo ya nishati ya nyuklia.
Mpango wa Iran bomba litoke Iran kupeleka gas Pakistan halafu liunganishwe mpaka China kupitia mradi unaomilikiwa na kufadhiliwa na China wa Ukanda mmoja njia moja ambao Marekani inaufanyia fitna kinoma noma ili kumharibia China na Iran na ndio sababu kubwa Donald Trump kutaka kuutumia mgogoro wa Kashmir kama msuluhishi wa Pakistan dhidi ya India ili apate pa kuingilia kwa kucheza na washirika wa Urusi na China ambao ni India na Pakistan kwa manufaa yake.
Kumbuka India na China ni maadui kwa kugombea mipaka ya maeneo ya Aksai Chin huko Ladakh na sehemu ya Kashmiri ambapo China alichukua asilimia 15 ili kulinda njia za kugikika kirahisi katika maeneo ya nyanda za juu za majimbo ya Hellojiang na Tibet huku Pakistan akimega asilimia 35 na India 50 pale kwenye Line of Control ya jimbo la Kashmir. Na usisahau kuwa Pakistan na india ni maadui wakubwa wakigombe jimbo la Kashmir na usisahau pia Urusi ni mshirika wa India na China huku Marekani nj adui wa Urusi na China huku akijaribu kuurejesha ushirika wake na India kwa kasi kutokea kwenye uchumi kwenda kwenye kijeshi kwa kutumia fursa za mizozo ya mipaka na China na umiliki wa usimamizi mkuu wa bahari ya China. Usisahau kuwa wahusika hawa wa Urusi Marekani India Pakistani na China wanamiliki silaha za nyuklia hivyo mzozo mkubwa baina yao au washirila wao ni tishio la ulinzi na usalama wa dunia nzima kama siyo mwanzo wa vita vikuu vya tatu vya dunia iwapo mizozo yao haitadhibitiwa mapema kwa weledi hekima na diplomasia ya hali ya juu katika upatanishi na usuluhishi.
Unaweza usielewe huu mnyororo ila jua kuwa cheche ikitokea sehemu moja itasambaza moto kote kama diplomasia na ujasusi visipotumika kudhibiti mgogoro na uzuri Marekani yeye kwake ana faida kuu mbili akinufaika kupata maslahi ni faida na akiwafarakanisha wakapigana pia kwake ni faida.
Umechoka ehh maana siyo kwa kukuzurulisha huku sasa turudi nyumbani maana kumenoga sasa kuiangusha Syria ili kuuondoa ushawishi wa Urusi kwa kumuondoa Bashar Assad na kuwaweka vibaraka wao ndo ulikuwa mkakati wa kwanza wa Marekani na baada ya kumuondoa Assad ingefata mkakati wa pili wa kuibana Urusi na Irani kwa kukata mirija ya pumzi zao za kiuchumi siasa jamii na utawala ila ngoma ikatibuka mwishoni.
Japo wajanja wanajua fika Urusi alishaanza kujiandaa kitambo kupigania uchumi jamii utulivu wa siasa zake kupitia zuio la kuanguka kwa Syria na Iran na sio hao tu hata China nae maana China ana mkakati wa kuwa dola kuu duniani kiuchumi na anajua fika injini ya ukuaji wa uchumi ni viwanda na hakuna viwanda bila usambazaji wa uhakika wa mafuta na gas hivyo ana mkakati mkubwa wa kuifanya Iran ndo iwe Saudi Arabia yake kama alivyofanya Marekani na si hivyo tu ana mkakati wa kuisambaza pesa yake ya Yuan ije kuwa kama dola hivyo anahitaji kupita ile njia iliyoasisiwa na kina Henry Kissinger ya kuijenga Petro dollar kupitia Saudi Arabia na China kwa sasa anaijenga Petro Yuan kupitia Iran kutumia ushawishi wake kuhodhi na kujihakikishia mnufaiko wa mafuta na gas ya Iran kama hujui rejea mikopo ya mabilioni ya dollar aliyoitoa China kwa Iran hivi karibuni au rejea mabadilisho ya sheria ya Irani yaliyofanywa na baraza la Maulamaa la Iran ili kuruhusu kampuni kuu za Taifa za nishati za China kuchukua hisa katika makampuni ya Taifa ya Nishati ya Irani pamoja na kuwekeza mabiioni ya dola na teknolojia katika miradi ya mafuta na gas ya Iran.
Kama bado hujaelewa jiulize kwa nini vikwazo vya Marekani kwa Urusi na Iran vinalalamikiwa kukosa matokeo makubwa kama ilivyopaswa jibu ni moja tu China inatumia nguvu zake za mitaji na teknolojia kuwekeza katika chumi za nchi hizo ili inufaike na mikataba ya usambaziwaji wa nishati za mafuta na gas kwa ajili ya kupanua uchumi wake wa viwanda na kupunguza matumizi ya nishati chafuzi za mazungira kama makaa ya mawe kwa viwanda vyake ambavyo yanailetea athari nyingi na kupunguza juhudi za China kuwa Clean and Smart economy kama ilivyo Ujerumani.
Japo kwa Urusi China anapata pia teknolojia za silaha nishati za nyuklia ushirika wa ulinzi wa kijeshi na kujifunza mambo mengi huku yeye akimwaga mafedha ya mitaji na teknolojia za kisasa kama vile akili bandia avionics digital technology technolohia za uzalishaji viwandani ujenzi wa miundombinu mifumo na vifaa vya kisasa vya ndege na masoko makubwa ya China ya bidhaa adimu za viwanda na kilimo nishati vinu vya nyuklia silaha mitaji ambapo vikwazo vya Marekani na Ulaya zililenga kuzibana kampuni za Urusi hivyo kuzitoa katika ushindani wa kidunia na kuua uchumi wa Urusi ili kupunguza utanukaji wake kidunia ili aje abanwe vizuri na kuongezeka kwa harakati za NATO halafu mwisho New World Order ikose mpinzani maana baada ya Urusi kubanwa kama wangefanikiwa angefata China afu tuone kama hizo mbwembwe na kelele za North Korea na Iran mngezisikia nyie wapenzi wakubwa wa siasa za kishabiki bila kuchunguza maana wengi wenu huamini Speaker ndo chanzo cha Sauti na ujumbe badala ya kujua nani anaongea nyuma ya Microphone.
Sasa bhasi unapoona Trans Siberian Gas pipeline, Turkish Stream, Nord Stream 1 na Nord Stream 2 Russia Mongoli China trilateral gas pipeline initiative na mengineyo jua ni mapambano ya uchumi kwa manufaa ya siasa .Ila mimi namuonea huruma Zelensky na Ukraine yake maana Urusi inataka kuikausha Ukraine ili iichukue tena kwa kutengeneza miundo mbinu mingine ya mabomba ya gas kwenda Ulaya bila kupitia Ukraine jambo ambalo litaikosesha Ukraine mabilioni ya dola na gas za bei chee kama mnufaiko wa usafirishaji wa gas ya Urusi kupitia kwao na kibaya zaidi si mabwana wakubwa wakina George Soros wala USA au EU wenye uwezo wa kuwapa kifurushi cha mpunga ruzuku wala mkopo wa kufidia hasara za hatua hiyo ya Urusi kwa Ukraine.
Na ndio maana wanajitahidi mno kuisihi Marekani Poland Ulaya zizuie juhudi hizo japo kiuhalisia ni ngumu na athari ya hatua hii ni kuudororesha kama siyo kuua zaidi uchumi wenye kifaduro na mkwamo wa siasa za Ukraine kitu ambacho kitachochea hali mbaya ya maisha na migogoro maandamano na ukosefu wa uungwaji mkono kwa walio wanasiasa na ma oligarch wanaohodhi maamuzi kwa sasa na kiuhalisia ikishafika hali hiyo ndipo Urusi itamsogeza mtu wao na kundi lao lirudishe utawala wao dhidi ya Ukraine ulioangusha na Orange Maidan revolution.
Warusi wanapiga pote pote kuanzia kuiandaa Donetsk na Lugansk kujitoa dhidi ya udhibiti wa Ukraine kupitia vita ama makubaliano kama ya Minsk accord au kura ya maoni ambayo itaipa maeneo hayo uhuru na haki ya maamuzi yao ya ndani kutoingiliwa na serikali kuu ya Ukraine na hili litakuwa chaguo la mwisho endapo tu watashindwa kujitoa na kuanzisha nchi zao huru zinazojitegemea . Kwa Urusi huu utakuwa ushindi kwa kufanikiwa kutanua ushawishi wao na onyo kuu kwa nchi yoyote ya karibu na Urusi itakayokubali kutumika na Marekani kuhujumu maslahi ya Urusi kuwa Urusi haitakubali kuhujumiwa kizembe bali itaiharibu nchi hiyo kwa vita uchumi na kuivunja kimaeneo na jamii kama walivyofanya kwa Ukraine kwa kuipoka udhibiti wa Crimea Lugansk Dinetsk na sasa wanaenda kuimalizoa mapato ya mabomba yake ya gas na kuuharibu utulivu wa uchumi na ustawi wa umma ili Waukraine wakafanye kazi za ushambaboy gereji na kufagia huko Ulaya Magharibi huku wakikutana na sera kali za uhamiaji za Ujerumani Uingereza na Ufaransa pamoja na ubaguzi wa hali ya juu ambako watapata kushika akili ya athari za kukubali kutumika na kukurupukia ajemda za madola makubwa bila kujiandaa na kutafakari athari zake kwa kina.
Siasa za wenzetu ni mbinu akili fitna na mikakati kuntu hadi unacheka ukiziangalia kukurukakara za siasa uchwara za Wabongo na Afrika
Kama kweli umesoma yote hii na kuielewa bila kuruka ruka wala kupagawa wala kukasirika bhasi we kweli noma ile kinomanoma
Contact +255 656264627
nicksonmbatina@gmail.com
Ikitokea umeisambaza sharti usiihariri na uonyeshe utambulisho wa muandaaji.
Ubongo wa Mbongo
Ndimi Nick Mbatina.

Comments

Popular posts from this blog

FAIDA ZA KUOA MKE ALIEKUZIDI UMRI

HISTORIA YA KHALIFA WA PILI SAYYIDNA OMAR (R.A)

Elimu kwa wanawake