Chanzo cha ajali ya lori kuwaka moto ni mtu mmoja alipojaribu kuiba betri

LORI LA MAFUTA LAPINDUKA MOROGORO, LALIPUKA NA KUUA ZAIDI YA 100
Ínaripotiwa kuwa Idadi kubwa ya watu wanaokadiriwa kuwa zaidi ya 100 wanahofiwa kufa moto baada ya gari la mafuta lililopata ajali kuwaka moto mkoani Morogoro.
Imeripotiwa kwamba Lori hilo lililokuwa limebeba mafuta lilikuwa linatokea Dar Es Salaam lilipofika eneo la Itigi Mzambarauni nje ya mji wa Morogoro muda ya saa moja asubuhi kukawa na mwendesha bodaboda akakatiza mbele ya lori hilo wakati mwenye lori anamkwepa ndipo lori hilo likaanguka upande wa kushoto mwa barabara, kisha akajitokeza mtu mmoja kuchomoa betri kwenye lori hilo, watu mbalimbali haswa wakiwemo waendesha boda boda nao wakafika eneo la tukio kwa ajili ya kuiba mafuta moto ukalipuka na wakapoteza maisha watu zaidi ya 100.
Mashuhuda wa tukio hilo wameviambia vyombo vya habari kuwa lori la mafuta (petroli) lilipinduka, hivyo watu mbalimbali, wengi wao wakiwa madereva wa pikipiki wakaenda eneo la tukio na vibebeo kwa lengo la kupata kuchukua mafuta.
Maafisa wa polisi wamesha wasili eneo la tukio kwa ajili ya kubaini idadi ya watu waliopoteza maisha. Kwa hakika huu ni msiba mwingine mkubwa kwa taifa letu,
Miili 60 imepokelewa Mochwari huku watu 70 wakiwa ICU wengine wakiwa na matatizo ya macho hawaoni.
R. I. P ndugu zetu

Comments

Popular posts from this blog

FAIDA ZA KUOA MKE ALIEKUZIDI UMRI

HISTORIA YA KHALIFA WA PILI SAYYIDNA OMAR (R.A)

Elimu kwa wanawake