Mwanamke mmoja ajipasua tumbo kumtoa mtoto

Mwanamke mjamzito ajifanyia upasuaji na kutoa mtoto Tanzania

Mwanamke mja mzitoHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Mwanamke mmoja anadaiwa kujipasua tumbo kwa kitu chenye ncha kali na kumtoa mtoto, wilayani Nkasi mkoani Rukwa Kusini Magharibi mwa Tanzania.
Tukio hilo limevuta hisia za wengi na wengine wakiwa katika taharuki wengi wakifika katika kituo cha afya kushuhudia ukweli wa tukio hilo linalodaiwa kutekelezwa na bi Joyce Kalinda.
Wakati taarifa za awali zikisema kuwa mwanamke huyo alijipasua umbo, Mganga mkuu wa wiaya ya Nkasi Dokta Hashi Mvogogo alizungumza na gazeti la Habari Leo alisema bado uchunguzi unafanyika ili kujua ukweli wa kilichotokea kwa mama huyo.
Uchunguzi unafanyika kubaini kama alijifanyia upasuaj mwenyewe kutoa mtoto au kuna mtu mwingine alifanya hivyo.
Daktari huyo amesema saa tisa alfajiri ya kuamkia siku ya Alhamisi, mwanamke huyo alifika katika kituo cha afya cha Kirando na kuanza kupiga kelele, akimtaka muuguzi aliyekuwa zamu ampe huduma za kumsaidia kujifungua.
Alisema kutokana na kuwepo kwa wagonjwa wengine kituoni hapo, muuguzi alimshauri mama huyo mja mzito kusubiri kidogo kisha alikwenda kumhudumia mgonjaw mwingine, lakini aliporejea mahali apokuwepo hakumkuta.

Kwa mujibu wa Dokta Mvogogo,ilipotimu alfajiri saa 11 mja mzito huyo alirudishwa hospitalini hapo akiwa amepasuka sehemu ya tumbo, huku watu waliomfikisha hospitalini hapo wakiwa wamembeba mtoto mchanga.
Watu hao walisema mwanamke huyo alikua amejipasua tumbo na kumtoa mtoto tumboni.
''Tumbo lilionekana limepasuliwa na kitu chenye ncha kali.Alipofika aliwekewa dripu tatu za damu ili kuokoa maisha yakekwani alikua amepoteza damu nyingi, lakini pia mtoto alipewa matibabu kutokana na kutolewa tumboni bila kufuata utaalamu unaotakiwa na sasa wote wanaendelea vizuri na matibabu,'' Dokta Mvogogo aliiambia Habari Leo.
Dokta Mvogogo amesema tukio hilo limeripotiwa polisi ili uchunguzi wa kina ufanyike kubaini ni nini kilichotokea kwa mama huyo.
Polisi nchini Tanzania wamethibitisha kuwepo kwa tukio hilo.Akizungumza na BBC kamanda wa Polisi mkoani Rukwa Mathias Nyange amethibisha tukio hilo
''Uchunguzi unaofanywa pia unahusisha mtaalamu wa magonjwa wa akili ambaye tunataka achunguze ili kubaini kama mama huyo ambaye huo ni uzao wake wa nane ana ugonjwa wa akili au la,'' alieleza Daktari huyo

Comments

Popular posts from this blog

FAIDA ZA KUOA MKE ALIEKUZIDI UMRI

HISTORIA YA KHALIFA WA PILI SAYYIDNA OMAR (R.A)

Elimu kwa wanawake