Skip to main content

Wahamiaji kutoka Amerika ya Kati wakijaribu kuingia marekani

 


Wachezea kichapo wakitaka kwenda Marekani

Msafara wa wahamiaji kutoka Amerika Kusini uliokuwa ukielekea nchini Marekani umekutana na marungu na gesi za kutoa machozi nchini Guatemala, ambako vikozi vya usalma vilifunga njia yao ya kupita kuelekea Marekani.

Maelfu ya watu walizuiwa kwenye barabara karibu na mpaka wa Guatemala na Honduras. Serikali imesema haingekubali “matembezi ya umati wa watu kinyume cha sheria “.

Wahamiaji wanaokadiriwa kuwa 7,000 , wengi wao kutoka Honduras, wameingia katika siku za hivi karibuni, wakikimbia umasikini na gasia.

Wanatumaini kusafiri hadi Mexico, na baadaye kuufikia mpaka wa Marekani.

Kila mwaka, maelfu ya wahamiaji wa Amerika ya kati hujaribu safari hii ili kujaribu kufika Marekani, mara nyingi kwa hutemea kwa miguu.

Rais mteule wa Marekani Joe Biden, kutoka chama cha Democrat, ameapa kuondoa sera kali za uhamiaji zilizowekwa na mtangulizi wake, Donald Trump, kutoka Republican.

Lakini utawala wa Bw Biden ,ambao utachukua mamlaka Jumatano, umewaonya wahamiaji kutofanya safari , kwasababu sera za uhamiaji hazitabadilishwa haraka.

Nini kilichotokea wakati msafara wa wahamiaji ulipoingia Guatemala?

Wakati wahamaiaji walipokuwa wakivuka mpaka wa Guatemala kuelekea kwenye mpaka wake na Mexico, walizingirwa na vikosi vya usalama karibu na kijiji cha Vado Hondo kilichopo kusini -mashariki.

Kikundi cha wanajeshi na maafisa wa polisi kilifunga barabara , na kuwazuia wengi wao kuendelea na safari. Baadhi ya wahamiaji hao bado walilazimisha kwa nguvu kupita, na kuwafanya maafisa wa usalama kuwasukuma nyuma.

Video iliyosambazwa kwenye mitandao ya kijamii, inaonesa vikosi vya Guatemala vikitumia gesi za kutoa machozi, vifaa vya kujikinga na marungu kuwarudisha nyuma wahamiaji. Watu kadhaa walijeruhiwa katika tukio hilo.Several Guatemalan soldiers clash with Honduran migrants at a police control in the city of Chiquimula, Guatemala

Takriban wahamiaji 7,000, wengi wao kutoka Honduras, wanakadiriwa kuwasili nchini Guatemalatangu IjumaaHondurans taking part in a new caravan of migrants set head to the United States, clash with Guatemalan soldiers as they try to cross into Guatemalan territory, in Vado Hondo, Guatemala

Polisi na wanajeshi wakitumia fimbo kuwawachapa wahamiaji ili kuwalazimisha kurudi walikotoka

Wahamiaji wengi walirudi nyuma na kuweka kambi, huku baadhi wakisubiri karibu na mpaka ili kujaribu tena bahati yao ya safari ya kuelekea nchini Marekani baadaye . Wengine walitorokea kwenye milimo iliyopo karibu na kujificha huko.

“Kwa bahati nzuri, vikozi vyetu vya usalam viliweza kudhibiti vita hivi ,” Guillermo Díaz, mkuu wa shirika la uhamiaji la Guatemala , aliliambia gazeti la New York Times “Tuliweza kutuliza kila kitu katika hali tatanishi sana .”

Taarifa kutoka ofisi ya rais wa Guatemala zinasema kuwa : “ujumbe wa Guatemala ni wa wazi: Haina hizi za matembezi ya wahamiaji haramu wanaosafiri kwa makundi ya watu wengi hayatakubalika, hii ndio maana tunashirikiana kwa pamoja na mataifa jirani kutatua tatizo hili kama suala la kikanda .”

Ni kwanini kuna idadi kubwa ya watu wanaokuja sasa?

Wahamiaji wanasema mateso, gasia na umasikini nidio hali halisi ya maisha wanayoishi kila siku katika mataifa yao. Hali zimekuwa mbaya hata zaidi kutokana na vimbunga vikubwa ambavyo viliyapiga maeneo ya Amerika ya kati mwezi Novemba mwaka jana.

Kwahiyo, katika kutafuta maisha bora, wanataka kufika Marekani kwa matumaini ya kupata kazi na usalama.Hondurans taking part in a new caravan of migrants set to head to the United States, take a break in Vado Hondo, Guatemala

Wahamiaji wanakimbia umasikini na gasia katika mataifa yao

Dania Hinestrosa, mwenye umri wa miaka 23 ambaye anasafiri na binti yake, aliliambia shirika la habari la AFP: “hatuna kazi, hakuna chakula, Kwahiyo niliamua kwenda Marekani .”

Ahadi ya sera mpya za uhamiaji chini ya utawala wa Biden pia inadhaniwa kuwachochea baadhi ya wahamiaji kufanya jaribio la kuufikia mpaka wa Marekani.

Utawala wa Marekani unaoingia madarakani unasema nini ?

Maafisa wa Bw Biden wamekwisha waonya wahamiaji wa America ya Kati wasifanye safari za hatari kuelekea kwenye mpaka wa Marekani.

Akizungumza na shirika la habari la NBC afisa wa Bw Biden ambaye jina lake halikutajwa alisema wahamiaji wanaojaribu kudai ukimbizi nchini Marekani “wanahitaji kuelewa kuwa hawataweza kuja Marekani mara moja “.

Utawala wa Biden utawapa kipaumbele wahamiaji wasio na vibali ambao tayari wanaishi nchini Marekani, sio wale wanaoelekea nchini humo kwa sasa, afisa huyo alisema.

“Uwezo wa mchakato kwenye mpaka sio kama mwangaza kiasi kwamba unaweza kuuwasha na kuuzima ,” Susan Rice, mmoja wa washauri wa Bw Biden wa sera. Aliliambia shirika moja la habari la habari za kihispania- Efe mwezi Disemba.

“Wanaoomba Uhamiaji na ukimbizi wanapaswa kutoamini kabisa wale wanaowaambia kuwa mipaka itafunguliwa ghafla kushugulikia kila mtu kuanzia siku ya kwanza. Haitakuwa hivyo .”

Mark Morgan, naibu kamishna wa forodha na ulinzi wa mpaka , wiki iliyopita aliwaambia wale watakaokua wahamiaji kwenye mpaka wa kusini mwa Marekani “usipoteze muda na pesa zako “.

Wajibu wa Marekani wa “utawala wa sheria na afya ya umma” hautaathiriwa na mabadiliko ya utawala, alisema katika taarifa.Mwanaume mlemavu akitembea kutoka Hondurus kuelekea Marekani

Mwanaume mlemavu akitembea kutoka Hondurus kuelekea Marekani

Misafara makumi kadhaa, baadhi ikiwa ya maelfu ya watu wameondoka kutoka Amerika ya kati katika miaka ya hivi karibuni. Kundi kubwa zaidi lilitoka Hondurus mwezi Oktoba mwaka 2018, na kumfanya rais Trump kusema “ani uvamizi”.

Lakini wote wamempinga Bw Trump, ambaye aliziwekea shinikizo nchi za Mexico, Guatemala, Honduras na El Salvador kwa kuwakamata wa wahamiaji haramu kaskazini mwa nchi.

Related Articles

Back to top button
VIEW

Comments

Popular posts from this blog

FAIDA ZA KUOA MKE ALIEKUZIDI UMRI

HISTORIA YA KHALIFA WA PILI SAYYIDNA OMAR (R.A)

Elimu kwa wanawake