UTURUKI YANUNUA SILAHA HATARI ZAIDI DUNIANI KUTOKA URUSI

Uturuki kununua mfumo wa kujilinda dhidi ya makombora wa S-400 kutoka Urusi licha ya pingamizi ya Marekani

Mfumo huo wa S-400 ni mojawapo wa silaha kali ya ardhini dhidi ya makomboraHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionMfumo huo wa S-400 ni mojawapo wa silaha kali ya ardhini dhidi ya makombora
Rais wa Uturuki Reccep Tayyep Erdogan amesema kuwa ana matumaini kwamba mfumo wa kujilinda dhidi ya makombora wa Urusi ambao Washington unauona kama tishio kwa ndege za Marekani utawasilishwa nchini humo mwezi Julai.
Marekani imesema kuwa Uturuki haiwezi kuwa na mfumo huo wa S-400 pamoja na ndege za kivita za Marekani aina ya F-35.
Lakini bwana Erdogan amesema kuwa Uturuki itamwajibisha mtu yeyote atakayeiondoa kutoka kwa mpango huo wa ununuzi wa ndege za F-35
Uturuki ambayo ni mwanachama wa Nato imetia asaini ya kununua ndege 100 aina ya F-35 na imewekeza vya kutosha katika mpango huo wa F-35.
Kampuni za Uturuki huzalisha vipande 937 za ndege hizo.
Bwana Edogan alisema kuwa anatumai kutatua hali hiyo na Marekani kupitia njia za kidiplomasia kabla ya mktano na rais Trump mwisho wa mwezi Juni, kulingana na chombo cha habari cha Reuters.
Ndege za Marekani aina ya F-35Haki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Uturuki imekuwa ikipigania sera ya ulinzi ya kuwa huru na imeimarisha uhusiano wake na Urusi kufuatia kuharibika kwa uhusiano wake na Marekani pamoja na mataifa ya Ulya.

Je Marekani imekuwa ikiiambia nini Uturuki?

Kaimu waziri wa ulinzi nchini Marekani Patrick Shanahan wiki iliopita aliiandikia Uturuki kwamba Marekani imesikitishwa kusikia kwamba wanajshi wa Uuruki wametumwa Urusi kujifunza mfumo huo wa S-400
Afisa mwengine mwandamizi kutoka Marekani katika wizara ya ulinzi Ellen Lord, aliambia maripota kwamba Marekani haikutaka maafisa wa kiufundi wa Urusi kuweza kuona udhaifu wa F-35.
Maafia wa Marekani badala yake walikuwa wakitaka Uturuki kununua mfumo wake kujilinda dhidi ya makombora wa Patriotic Missile.
Uturuki ina jeshi la pili kwa ukubwa katika Nato, muungano wa kijshi wa mataifa 29 ulioanzishwa kujilinda dhidi ya kile kilichoitwa kuwa Muungano wa Soveiti wakati huo.

S-400 ni mfumo wa aina gani?

S-400 au "Triumf" ni moja ya silaha ya hali ya juu duniani inayotoa ulinzi wa ardhini na angani.
S-400 moja ina uwezo wa kuangusha makombora 80 yaliyorushwa umbali wa kilomita 400 kwa wakati mmoja.
Urusi inasema kuwa ina uwezo kuangusha makombora yanayorushwa kutoka kwa ndege zisizo na rubani na makombora ya masafa marefu.

S-400 inafanya vipi kazi?

Mchoro wa mfumo wa kujilinda dhidi ya makombora S-400
Image captionMchoro wa mfumo wa kujilinda dhidi ya makombora S-400
  • Ni kifaa kilicho na uwezo wa kutoa taarifa kwa gari maalum linaloelekezwa katika eneo linalolenga kushambuliwa
  • Taarifa hizo zinatumwa kwa gari linalosaidia kurusha makombora na kuelekeza makombora angani
  • Kifaa hiki pia kinasaidia kuelekeza makombora katika eneo maalum

Comments

Popular posts from this blog

FAIDA ZA KUOA MKE ALIEKUZIDI UMRI

HISTORIA YA KHALIFA WA PILI SAYYIDNA OMAR (R.A)

Elimu kwa wanawake