TIMU ITAKAYOGOMEA MECHI KURUSHWA LIVE ITAHESABIKA HAIKUFIKA UWANJANI=TFF

TFF YAIONYA PAMBA"TIMU ITAKAYOGOMEA MECHI KURUSHWA LIVE ITAHESABIKA HAIKUFIKA UWANJANI"
Mechi za play off kati ya Pamba SC vs Kagera Sugar FC, na Geita Gold FC vs Mwadui FC zilizokuwa zichezwe (Juni 2) zimesogezwa mbele hadi ( Juni 3 ) kutokana na sababu za kiusalama.
Taarifa hiyo imetolewa na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) ikieleza kuwa usalama wa magari ya Azam TV ulikuwa mdogo kutokana na baadhi ya mashabiki kutishia kuvunja vioo wakipinga mechi hizo kuoneshwa moja kwamoja.
Kwa mujibu wa TFF, mechi hizo zote zikiwemo za marudiano zitakazochezwa Juni 8, 2019 zitaoneshwa moja kwa moja ( live ) na kituo cha Televisheni cha Azam TV.
“Kwa mujibu wa kanuni za ligi, haki za matangazo ya televisheni ni mali ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF). Timu itakayozuia mechi yake kuoneshwa, itahesabika kuwa haikufika uwanjani, hivyo itachukuliwa hatua kwa mujibu wa kanuni,” imeeleza sehemu ya taarifa hiyo ya TFF.
Aidha TFF imewataka viongozi wa timu husika kuepuka kutoa matamko ambayo ni kinyume na kanuni za mpira wa miguu na kusisitiza kuwa watakaokwenda kinyume watachukuliwa hatua za kinidhamu na kimaadili.

Comments

Popular posts from this blog

FAIDA ZA KUOA MKE ALIEKUZIDI UMRI

HISTORIA YA KHALIFA WA PILI SAYYIDNA OMAR (R.A)

Elimu kwa wanawake