RAISI WA UTURUKI ERDOGAN ASHIRIKI SALA YA GHAIB YA JENEZA KIFO CHA RAISI WA ZAMAN WA MISRI WA CHAMA CHA MUSLIM BROTHERHOOD
Rais Erdoğan ashiriki sala ya jeneza, kifo cha Mohamed Morsi
Rais wa Uturuki ashiriki sala ya jeneza ya kifo cha rais wa zamani wa Misri Mohamed Morsi
Rais Erdoğan akemea ukimya wa ulimwengu wa Magharibi kwa kufumbia macho kupinduliwa kwa rais Morsi na kuzuiliwa kwake huku haki zake za msingi zikidhulumiwa hadi kupelekea kifo chake.
Hayo rais wa Uturuki ameyazungumza hayo katika mkutano wa hadhara mbelel ya hospitali ya Sultangazi Haseki mjini Istanbul.
Kwa mara nyingine rais wa Uturuki ametoa salamu za rambi rambi kwa raia wa Misri kwa kumpoteza kiongozi shujaa.
Sala ya jeneza imefanyika mjini Istanbul, Yerusalemu na maeneo mengine ulimwenguni.
Mjini Ankara, mkurugenzi wa idara ya masuala ya kidini Uturuki Ali Erbaş ameongoza sala ya jeneza katika mskiti wa Hacı Bayram Veli.
Viongozi tofauti wameshiriki katika sala hiyo akiwemo waziri wa sheria .
Comments
Post a Comment