NUHU JABIR MRUMA AWA KATIBU MKUU BAKAWATA


Ofisi ya M
Hatimaye
Nuhu Jabir Mruma aukwaa ukatibu mkuu BAKWATA.
....................................
Mwalimu Nuhu mzaliwa wa kijiji cha Shighatini kilichoko kwenye kilele cha milima ya Upare wilayani Mwanga mkoani Kilimanjaro ameanzia kwenye unaibu katibu utawala, ukaimu katibu na leo kwenye Baraza la Idil Fitri ametangazwa kuwa katibu mkuu.- BAKWATA.
Nuhu Mruma ambaye miaka miwili nyuma alikuwa Mwalimu mkuu shule ya sekondari Alharamain ya jijini Dar es salaam amefahamika sana kwa kasi ya utendaji wake.
Tangu alipopewa unaibu katibu, BAKWATA ilikuwa inapita kwenye kipjndi kigumu ambacho kilihitaji mchapa kazi jasiri mwenye kujituma aliyekuja BAKWATA kwa ajili ya kuisaidia na si vinginevyo.
Nuhu Mruma anafahamika kwa msimamo wake wa kuheshimu kazi za watendaji huku akiamini kwamba "BAKWATA haihitaji viongozi bali BAKWATA inahitaji watu"
Bila shaka anamaanisha viongozi wapo na kazi yao ni kuhudumia watu na kutafuta uungwaji mkono.
Anaamini kazi ya kwanza ya kiongozi ni kukusanya na kuunganisha watu. Na wala jukumu la kiongozi siyo kufanya juhudi za kuendelea kushikilia nafasi ya uongozi.
Zaidi ya hapo anapenda Mufti na BAKWATA itajwe vizuri. Anawapenda sana wafanyakazi wanaoiwezesha BAKWATA kuwa karibu na watu.
Pia anfanya juu chini kujenga uhusiano mwema baina ya BAKWATA na serikali yetu tukufu na asasi zake pamoja na jumuia za kiraia za ndani na nje ya nchi.
Pia ana uhusiano mzuri sana na wafanyakazi wa BAKWATA makao makuu pamoja na wanahabari wa vyombo mbalimbali.
Kwa ujumla mwalimu Nuhu anatafsiri kivitendo sera, mitazamo na kauli mbiu ya mufti ya :-
"JITAMBUE , BADILIKA, ACHA MAZOEA"
Kwa kufanya hivyo Nuhu anamsaida mufti Zubeir kujenga "BAKWATA MPYA" inayoongoza waislamu wa Tanzania wakiwa safu moja bila kujali madhehebu au taasisi zao.
Alipoteuliwa kuwa kaimu katibu wafanyakazi wa BAKWATA makao makuu walipata matumaini mapya na makubwa sana.
Bila shaka sasa watapata nguvu mpya.
Sote tuonbe mola ampe busara zaidi, huruma nyingi, utu, hekima na maarifa makubwa zaidi ili awe msaidizi mwema wa mufti wa Tanzania.
.................
Harith Nkussa
Mwandishi maalum wa mufti
Jumatano, saa moja na dkk 56 usiku
Makorora. Tanga

Comments

Popular posts from this blog

FAIDA ZA KUOA MKE ALIEKUZIDI UMRI

HISTORIA YA KHALIFA WA PILI SAYYIDNA OMAR (R.A)

Elimu kwa wanawake