KUMBUKUMBU:

Leo Juni 16 ni siku ya Mtoto wa Afrika.
Historia ya siku hii ilianza mwaka 1991 baada ya Umoja wa Afrika kuamua kuitangaza siku hii kwa ajili ya kuenzi watoto wa mji wa Soweto nchini Afrika Kusini waliouawa na askari wa Kikaburu mwaka 1976, waliokuwa wakiandamana wakipinga vitendo vya unyanyasaji na ubaguzi wa rangi uliokuwa ukiendelea, na pia kuhamasisha dunia kupinga vitendo vya kikatili kwa watoto.
Askari hao waliwafyatulia risasi na kuua watoto zaidi ya 170 na kujeruhi mamia wengine.
Tukio hili lilishtua dunia nzima na mpaka sasa limebaki kama kielelezo cha matukio mabaya yaliyotakana na ubaguzi wa rangi barani Afrika.
Pichani ni mtoto Hector Pieterson (13) ambaye ni miongoni mwa watoto waliouawa na askari wa Kikaburu, akiwa amebebwa na mwanafunzi mwenzake Mbuyisa Makhubo, pembeni akiwa na dada yake Antoinette ambaye mpaka sasa bado yuko hai.

Comments

Popular posts from this blog

FAIDA ZA KUOA MKE ALIEKUZIDI UMRI

HISTORIA YA KHALIFA WA PILI SAYYIDNA OMAR (R.A)

Elimu kwa wanawake