Esperance yatakiwa kurudisha kombe Klabu bingwa

Klabu bingwa Afrika: Esperance yatakiwa kurudisha kombeSaa 6 zilizopita

Wachezaji wa WydadHaki miliki ya pichaAFP
Image captionWachezaji wa Wydad walimgomea mwamuzi wakimtaka atumie VAR
Esperance wametakiwa kurejesha kombe la ligi ya klabu bingwa Afrika na kucheza mechi ya marudiano ya fainali.
Esperance ya Tunisia iliongoza kwa goli 1-0 kwenye mechi ya marudiano lakini wapinzani wao Wydad Casablanca waliondoka baada ya goli lao la kusawazisha kukataliwa
Wydad walitaka video ya wasaidizi wa waamuzi VAR kuthibitisha kama lilikua goli au la lakini mfumo wa mashine hiyo ulikua haufanyi kazi.
Shirikisho la soka Afrika (Caf) lilisema kuwa mechi ya marudiano itachezwa katika uwanja wa ugenini.

Matokeo hatimaye yalisimama kuwa 1-1 kutokana na mechi ya kwanza ya Morocco
Mechi ya marudiano itafanyika baada ya michuano ya kombe la mataifa Afrika itakayofanyika nchini Misri, itakayomalizika tarehe 19 mwezi Julai.
Taarifa ya Caf imesema ''taratibu za mchezo na usalama havikufuatwa'' kwenye mechi ya marudiano na kuweka wazi kuwa wachezaji wa Esperance lazima warejeshe medali za ushindi na kombe.
VARHaki miliki ya pichaAFP
Image captionWachezaji hawakujulishwa kama mashine ya VAR ilikua haifanyi kazi
Mchezo wa marudiano uliingia dosari baada ya Waydad kufikiri kuwa wamesawazisha dakika ya 59 kupitia goli la kichwa la Walid El Karti.Goli lilikataliwa kwa madai ya kuvunja sheria za mchezo.
Mashine ya VAR ilionekana kando ya uwanja lakini wachezaji hawakuelezwa kamailikua haifanyi kazi kazi.
EsperanceHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionEsperance ilipopata ushindi kabla ya ushindi kutenguliwa
Hatimaye mwamuzi akatoa ushindi kwa mabingwa mara tatu, Esperance baada ya dakika 95.
Rais wa Wydad amesema timu yake ''imeathirika'' na Caf ikaitisha mkutano wa kamati kuu ambao walitoa uamuzi wa kuwepo kwa mechi ya marudiano


Comments

Popular posts from this blog

FAIDA ZA KUOA MKE ALIEKUZIDI UMRI

HISTORIA YA KHALIFA WA PILI SAYYIDNA OMAR (R.A)

Elimu kwa wanawake