AMPA MTOTO WAKE WA KAMBO CHAKULA ALICHOKICHANGANYA NA HEDHI

Mshtuko !! Pichani mdada huyo Kwa jina la Annet Namata nchini Uganda amempa mtoto binti yake wa kambo chakula alichokichanganya na damu yake ya hedhi. Baada ya kula chakula hicho ambacho damu ya mdada huyo ilichanganywa na mchuzi wa mabiringanya mtoto huyo alianza kutapika mfululizo ambapo Annet alikuwa ameshatoka kwenda Kwenye mishe zake
Bahati majirani walimuona mtoto huyo akitapika mfululizo walipomfuata kumuuliza akawaonesha sahani ya chakula ambapo waliona vitu vya ajabu ndipo wakamtaarifu mume wa Annet anayeitwa Unusu Lungu. Baada ya kuja kujionea mume huyo alipatwa na hasira kali akamfuata mkewe huyo alipo kisha kuanza kukwaruzana
Awali, Annet Alijitetea kuwa mtoto huyo wa kike umri wa Shule ya msingi alichukuwa mwenyewe damu hiyo ya hedhi Kwenye ndoo akachanganya na chakula ale. Alieleza hayo baada ya yeye kulazimishwa ale chakula hicho ndipo akasema kina damu ya hedhi yeye hawezi kula
Alipobanwa zaidi Na mumewe Na mmoja wa viongozi wa kike wa eneo Hilo amekiri kumuwekea mtoto vitu hivyo akisema anaomba msamaha kwani mumewe alikuwa akimpenda sana mwanae kuliko yeye hata zawadi nyingi humnunulia mwanae kuliko yeye ndipo akapandwa Na hasira akafanya hivyo baada ya kuwaeleza mashoga zake ambao anadai Ndio walimshauri Annet achukue damu yake ya hedhi amuwekee mtoto huyo Kwenye chakula Ili awe mwendawazimu Ili yeye Na mumewe mahaba yao yachanue
Suala Hilo limefikishwa police Kwa hatua zaidi huku mtoto huyo akipatiwa Huduma za kiafya

Comments

Popular posts from this blog

FAIDA ZA KUOA MKE ALIEKUZIDI UMRI

HISTORIA YA KHALIFA WA PILI SAYYIDNA OMAR (R.A)

Elimu kwa wanawake