Afcon 2019: Wachezaji nyota wa timu za Afrika mashariki

Kombe la Afrika
Mataifa manne ya Afrika mashariki yamefuzu kwa kombe la mataifa ya bara Africa Afcon yatakayoanza ramsi nchini Misri namo tarehe 22 mwezi Juni .
Uganda iliibuka kidedea katika kundi lake huku Kenya, Tanzania na Burundi zikifuzu katika nafasi ya pili baada ya shirikisho la soka barani Afrika kuongeza timu kutoka 16 hadi 24 mwaka huu.
Mara ya mwisho ya eneo la afrika mashariki kuwakilishwa katika michuano hiyo ni 2004 wakati kenya na Rwanda walishiriki katika michuano ya Tunisia.
Wote waliondolewa katika droo ya kimakundi. Hii ni mara ya kwanza kwamba mataifa manne ya Afrika mashariki yanashiriki katika kombe la Afcon kwa pamoja.
Na hivyobasi shirika lako la habari la BBC limeamua kukuangazia kuhusu wachezaji nyota wa timu hizo za Afrika mashariki
Mbwana Samatta[ Nahodha Taifa Stars Tanzania}
Mbwana Aly Samatta alizaliwa Dar es Salaam, 7 Januari 1992.
Mbwana Aly Samatta alizaliwa Dar es Salaam, 7 Januari 1992.
Samatta alianza maisha ya soka katika klabu ya Africa Lion yenye makazi yake jiji la Dar-es-Saalam maeneo ya Mbagala.
Ni mchezaji wa soka wa Tanzania ambaye anacheza kama mshambuliaji katika klabu ya Genk nchini Ubelgiji na ni nahodha wa timu ya Taifa Stars ya Tanzania.
Kabla ya kujiunga na miamba ya soka nchini Ubelgiji alikuwa alikuwa katika kikosi cha timu ya soka nchini DR Congo TP-Mazembe iliyoshinda Ligi ya Mabingwa Afrika mwaka 2015, akifunga mabao saba na kuibuka mfungaji bora wa mashindano hayo.
Mnamo Januari 2016, alikuwa mchezaji wa kwanza kutoka Afrika mashariki kutwaa tuzo ya Mchezaji bora wa mwaka wa CAF anayechezea ndani ya Afrika.
Mbwana alipata pointi 127,akimshinda mchezaji mwenzake wa TP Mazembe Robert Muteba Kidiaba, ambaye amepata pointi 88.
Waghdad Bounedjah wa Algeria alishika nafasi ya tatu akiwa na pointi 63.
Pia Alifunga hattrick ya kukumbukwa kwa TP Mazembe dhidi ya Moghreb Tétouan ambayo ilipata nafasi katika mashindano ya fainali za CAF 2015.
Muda mfupi baada ya kushinda tuzo ya mchezaji bora anayecheza ndani ya Afrika, alisaini mkataba wa miaka minne na nusu katika klabu ya KRC Genk.
Tarehe 23 Agosti 2018 Samatta alifunga hat-triki dhidi ya Timu ya Brøndby IF katika Europa League kwa ushindi wa mabao matano kwa mawili.
Simon Msuva { Winga wa Taifa Stars Tanzania}
Simon Happygod Msuva alizaliwa 3 Desemba 1993 jijini Dar es Salaam, Tanzania.Haki miliki ya pichaFACEBOOK/MSUVA
Simon Happygod Msuva alizaliwa 3 Desemba 1993 jijini Dar es Salaam, Tanzania.
Ni mchezaji wa kandanda ambaye anacheza nafasi ya winga mshambuliaji katika timu ya Al Jadida kutoka nchini Morocco .
Amewahi kuwa mfungaji bora wa Ligi kuu ya Vodacom nchini Tanzania Bara kwa msimu wa 2014-2015 ambapo alifunga magoli 17.
Mwaka 2016-2017 aliibuka tena mfungaji bora akiwa na magoli kumi na nne.
Pia alikuwa mfungaji bora katika Kombe la Mapinduzi lililofanyika mwaka 2015 akifunga magoli manne.
Bwana Msuva amewahi kufanyiwa majaribio katika klabu inayoshiriki ligi kuu ya Afrika Kusini Bidvest.
Mwanzoni mwa mwaka wa 2017, aliingia mkataba kuichezea klabu ya Al Jadida ya nchini Morocco.
Msuva amekuwa kugonga vichwa vya habari katika Ligi hiyo kwa umahiri wake unaozidi kuimarika kila uchao.
Victor Mugubi Wanyama{ Nahodha wa Harambee Stars Kenya}
Victor Mugubi WanyamaHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Alizaliwa mwaka 1991 na alisomesa shule ya upili ya kamukunji inayosifika sana kwa uchezaji wa soka.
Ni mchezaji wa soka wa kulipwa wa Kenya ambaye anacheza kama kiungo mkabaji.
Akiwa nahodha wa timu ya taifa ya Kenya Mchezaji huyo anaichezea klabu ya Tottenham ya Uingereza.
Mbali na kuingoza timu ya Kenya Harambee Stars kufuzu katika komnbe la mataifa ya Africa ndiye Mkenya wa kwanza kabisa kufunga bao katika Ligi ya Mabingwa ya UEFA wakati alipoifungia Celtic ilipoishinda Barcelona 2-1 2012.
Alijiunga na ligi ya Uingereza 2013 akiichezea klabu ya Southampton kwa dau la £12.5 milioni hivyo basi kumfanya yeye kuwa mchezaji ghali zaidi kuwahi kuuzwa na klabu ya Scotland.
Tangu alipoanza kucheza kandanda ya kimataifa, Wanyama ameichezea timu ya taifa ya Kenya zaidi ya mara 30 kuanzia mwezi Mei 2007 akiwa na umri mdogo wa miaka 15.
Hivi majuzi alishirikishwa katika kikosi cha Tottenham kilichoshindwa na Liverpool katika fainali ya ligi ya mabingwa Ulaya.
Michael Olunga {Mshambuliaji hatari wa Harambee Stars Kenya}
Michael Olunga alizaliwa mnamo tarehe 26 mwezi Machi 1994.
Alizaliwa mnamo tarehe 26 mwezi Machi 1994.
Ni mchezaji wa kulipwa kutoka Kenya ambaye anaichezea klabu ya Japan ya Kashiwa Reysol na timu ya taifa ya Harambee Stars kama mshambuliaji hatari.
Akiwa mwanafunzi wa shule ya upili ya Upper Hill , Olunga alianza maisha yake ya kandanda kwa kujiunga na kikosi cha Liberty Academy katika ligi ya kaunti ya nairobi.
Aliifungia timu hiyo magoli 32 lkatika msimu wa 2012, akiwasaidia kumaliza msimu huo bila kufungwa kabla ya timu hiyo kupanda katika daraja la kaunti ya nairobla ligi ya kimikoa.
Alijiunga na klabu ya tusker kwa mwaka mmoja kabla ya kuelekea Thika United.
Baadaye alijiunga na mabingwa wa Lihi ya Kenya Gor Mahia ambapo alimaliza msimu huo na magoli 19 na kuisaidia timu hiyo kushinda taji lake la 15.
Tarehe 17 februari 2016 Olunga alijiunga na klabu ya Djurgadens IF kwa kandarasi ya miaka minne. Aliorodheshwa wa tano katika ufungaji wa magoli.
Mwaka 2017 Olunga alijiunga na klabu ya China Guizhou Zhicheng.
Mwezi Septemba 2017 Olunga aliichezea klaby ya la liga Girona kwa mkopo ambapo aliwahi kufunga hat-trick hyake ya kwanza dhidi ya klabu ya las Palmas.
Agosti 2018 alijiunga na klabu ya Japan ya kashiwa Reysol.
Emmanuel Okwi {Kiungo wa kati wa Uganda Cranes}
Emmanuel Okwi
Alizaliwa mjini Kampala, Uganda, mnamo tarehe 25 Disemba 1992.
Ni kiungo wa kati anayechezea klabu ya Simba S.C. ya Tanzania na timu ya taifa ya Uganda.
Aliichezea klabu ya Sports Club Villa ya Uganda kabla ya kuelekea katika klabu ya Simba ya Tanzania kwa dau la US$40,000.
Hatahivya klabu ya Tunisia Etoile du sahel ilimsaini kwa dau lililovunja rekodi la US$300,000.
Disemba 2013 alirudi SCvilla ya Uganda kabla ya kuhamia Simba ambapo 2015 alitia saini mkataba wa miaka mitano
Denis Onyango{ Nahodha na kipa wa Uganda Cranes}
Denis Onyango
Alizaliwa tarehe 15 Mwezi Mei 1985.
Ni mchezaji wa Uganda anayecheza soka yake ya kulipwa nchini Afrika Kusini akiichezea klabu ya Mamelodi Sundowns mbali na kuwa nahodha wa timu yake ya taifa Uganda Cranes.
Alianza maisha yake ya soka nchini Uganda kabla ya kuelekea Afriika Kusini ambapo alijiunga na timu ya Superport United, Mpumalanga Black Aces, na Mamelodi Sundowns.
Akiichezea Mamelodi Sundowns, alishinda taji la ligi ya mabingwa ya Caf 2016 na kushiriki katika kombe la FifaClub World Cup.
Alitangazwa mchezaji bora wa mwaka kutoka Afrika.
Pia aliorodheshwa kuwa kipa wa 10 bora duniani katika orodha ya mwaka 2016 ilioandalia na IFFHS {International Federation of Football History & Statistics}.
Fiston Abdul Razak {Mshambuliaji matata wa Burundi}
Fiston Abdul Razak alizaliwa tarehe 5 Septemba 1993.
Fiston Abdul Razak alizaliwa tarehe 5 Septemba 1993.
Ni mchezaji wa Burundian ambaye anaijezea klabu ya JS Kabylie na timu ya taifa ya Burudi kama Mshambuliaji
Kabla ya kujiunga na JS Kabylie, alifanikiwa kuzichezea klabu za LLB Académic FC, Rayon Sports F.C, CSMD Diables Noirs, Sofapaka F.C ya kenya , Mamelodi Sundowns F.C ya afrika kusini , Bloemfontein Celtic F.C, C.D. Primeiro de Agosto ya Angola na Al-Zawra'a SC.
Saido Berahino{ Mshambuliaji hatari wa Burundi}
Saido Berahino
Alizaliwa nchini Burundi tarehe 4 mwezi Agosti 1993.
Akiwa mchezaji wa kulipwa wa Burundia mbaye ara ya mwisho aikuwa mshambuliaji wa klabu ya Uingereza ya Stoke City na timu ya taifa ya Burundi.
Baada ya kutoka Burundi akiwa moto mdogo alipata uhifadhi wa kisiasa mjini Birmingham ambapo alisaidiwa kuingiliana na jamii ya Uingereza.
Berahino alijiunga na West Bromwich akiwa na umri wa miaka 11 na kuwa mchezaji wa kulipwa miaka saba baadaye. Aliichezea kwa mkopo klabu kama vile Northampton Town, Brentford na Peterborough United.
Allichezea mara ya kwanza klabu ya West bromwich albion katika msimu wa 2013-14 ambapo alifunga hattrick dhidi ya klabu ya Newport kaunti mbali na kufunga goli la ushindi dhidi ya Klabu ya Man United.
Katika msimu wake wa pilki alifunga magoli 20 kati ya mechi 45 katika mashindano yote.
Aliiwakilisha Uingereza katika mashindano yote ya vijana
Berahino aliiwakilisha Uingereza katika mashindano yote ya vijana kutoka umri wa miaka 16 hadi umri wa miaka 21 na alikuwa miongoni mwa kikosi cha wachezaji wasiozidi umri wa miaka 17 ambacho kilishinda ubingwa wa Ulaya.
Aliitwa kuiwakilisha Uingereza katika timu kuu 2014 lakini hakuchezeshwa.
Aliamua kuichezea Burundi mnamo mwezi Agosti na kufunga katika mechi yake ya kwanza.
Yannick Bolasie {Winga hatari wa DR Congo}
Yannick BollasieHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Yannick Bolasiealizaliwa tarehe 24 Mei 1989.
Ni mchezaji winga wa kulipwa anayeichezea klabu ya Anderlecht kwa mkopo kutoka timu ya Uingereza ya ligi kuu ya Everton.
Akiwa mzaliwa wa mji wa Lyon nchini Ufaransa, alizichezea klabu za Plymouth Argyle, Barnet, Bristol City, Crystal Palace na Aston Villa.
Bolasie ameichezea mara kadhaa timu yake ya taifa ya Democratic Republic of the Congo.
Alianza maisha yake ya soka na klabu ya Rudshden and Diamonds akiwa na umri wa miaka 16.
Alirudi nchini Uingereza 2008 baada ya kufanyiwa majaribio na timu ya Playmouth Argyle kabla ya kuandikisha kandarasi ya miaka miwili na klabu hiyo.
Mwaka 2012, Bolasie alitia saini kandarasi ya miaka mitatu na klabu ya Crystal Palace.
Mwaka 2016 mchezaji huyo matata aliijiunga na Everton kwa dau la uhamisho la £25m.
2018 Bollasie aliyekuwa na jeraha la muda mrefu na hata kumzuia kuichezea klabu yake ya Crystal Palace kwa muda mrefu alijiunga na klabu ya Aston Villa kwa mkopo kutoka Everton.
Katika msimu wa 2018-19 alijiunga na klabu ya Anderlecht.

Comments

Popular posts from this blog

FAIDA ZA KUOA MKE ALIEKUZIDI UMRI

HISTORIA YA KHALIFA WA PILI SAYYIDNA OMAR (R.A)

Elimu kwa wanawake