AFARIKI BAADA YA KUTUKANWA NA MWANAE

Polisi wilayani Nkasi katika mkoa wa Rukwa inamshikilia William Sokoni (33) akidaiwa kumtukana matusi ya nguoni mama yake mzazi, Clemensia Wangabo (77) na kumsababishia umauti. Mwanaume huyo ambaye ni mkazi wa kijiji cha Mtenga inadaiwa alighadhabika baada ya mama yake mzazi kumtaka amlipe kiasi cha Sh 50,000 alizomkopesha muda mrefu. Baada tu ya kumlipa alikwenda kumtukana na kumwambia mama yake kuwa ni heri yeye William angenyonya maziwa ya mbwa kuliko ya mama yake huyo, ndipo ghafla mama huyo akaanguka na kupoteza fahamu mbele yake na mkewe, mpaka umauti ukamkuta.
Toa maoni yako

Comments

Popular posts from this blog

FAIDA ZA KUOA MKE ALIEKUZIDI UMRI

HISTORIA YA KHALIFA WA PILI SAYYIDNA OMAR (R.A)

Elimu kwa wanawake