Wafahamu Malaika na kazi zao

WAFAHAMU MALAIKA NA KAZI ZAO.
πŸ‘‰JIBRIIL
Huyu ni Malaika mkubwa kabisaa kati ya Malaika wote aliyowaumba ALLAH (S.W.), Malaika huyu ana mbawa takribani 600. Kazi kubwa ya Malaika huyu ni kuteremsha Wahyi (ufunuo) kwa Mitume, tokea kwa Adamu (A.S.) mpaka Mtume wa mwisho Muhammad (S.A.W).
πŸ‘‰ MALAKUL MAUTI
Huyu ni Malaika maarufu sana kufahamika kwa watu wengi. Malaika huyu amepewa jukumu na ALLAH (S.W.) la kutoa Roho (Nafsi) za watu. Malaika huyu kapewa uwezo wa kuingia popote pale ili kutoa Roho ya mtu ambaye muda wake umeshafika wa kuondoka hapa duniani, hata kama mtu huyo awe na ulinzi kiasi gani. ALLAH amemtaja Malaika huyu kwenye Qur'an pale aliposema, "Sema: Atakufisheni Malaika wa Mauti aliyewakilishwa kwenu, kisha mtarejeshwa kwa mola wenu." Surat Assajida: 11.
πŸ‘‰ RAQIIB NA A'TIID
Hawa ni Malaika wawili mmoja anakaa upande wa kulia wa mwanadamu na mwengine anakaa upande wa kushoto wa mwanadamu. Kazi yao kubwa ni kuandika matendo (Amali) ya wanaadamu. Wa kulia anaandika matendo mema na wa kushoto anaandika matendo maovu. Popote utakapokwenda hawa Malaika unao, utakachosema au utakachofanya kiwe kibaya au kizuri hawa Malaika wanakiandika. ALLAH(S.W.) amewataja Malaika hawa kwenye Qur'an pale aliposema, " Hatoi kauli yoyote (mwanaadamu) isipokuwa karibu naye yuko mngojeaji tayari (kuandika)." Qur'an (50:18).
πŸ‘‰MUNKAR NA NAKIIR
Hawa nao pia ni Malaika wawili wanaopatikana katika maisha ya barzakh (Maisha ya kaburini). Na kazi yao kubwa ni kuwauliza watu maswali ndani ya kaburi baada tu ya kuzikwa kwao (mtu). Kama ulikuwa mwema hawatokudhuru, lakini kama ulikuwa muovu watakudhuru tu.
πŸ‘‰ISRAAFIIL
Huyu ni Malaika ambaye kazi yake kubwa ni kupuliza baragumu (parapanda) siku ya Qiyama. Inasemekana tokea aumbwe Malaika huyu hakuwahi kutoa pumzi nje, ila kazi yake ni kuingiza pumzi ndani. Atakuja kuitoa siku ya kiama pale atakapoamrishwa apulize baragumu siku ya Kiama.
πŸ‘‰MAALIK
Huyu ni Malaika wa motoni na kazi yake kubwa ni kuwaadabisha madhalimu na watenda maasi,maovu na machafu. Huyu malaika tangu aumbwe hajawahi kucheka wala kutabasamu, ila alikuja kutabasamu baada ya Mtume kufika mbinguni, na Mtume mwenyewe hakujua kama kaoneshewa tabasamu ambapo alimuuliza Jibriil (A.s.) mbona Malaika wote wanaonesha furaha juu yangu lakini mmoja tu haoneshi furaha, Jibriil akamwambia tena hapo katabasamu baada ya kukuona wewe kipenzi cha ALLAH (S.W.). Sasa jiulize mimi na wewe?. Tufanye toba kwa wingi na tumtii ALLAH na Mtume wake.
πŸ‘‰RIDHWAAN
Huyu ni Malaika wa peponi, na kazi yake kubwa ni kuwakaribisha waja wema kuingia peponi na kuwariwadha kutokana na mitihani waliyokutana nayo duniani.
πŸ‘‰MIKAAIL
Huyu ni Malaika mwengine ambaye kazi yake kubwa ni kuteremsha Mvua. Kila tone moja basi linawakilishwa duniani na Malaika mmoja wakiongozwa na Mikaail.
WABILLAHI TAWFIIQ.
KAMA KUNA SEHEMU NIMETEREZA MIMI NAYE NI BINADAMU, HAKUNA MKAMILIFU BALI UKAMILIFU NI WA ALLAH (S.W.).

Comments

Popular posts from this blog

FAIDA ZA KUOA MKE ALIEKUZIDI UMRI

HISTORIA YA KHALIFA WA PILI SAYYIDNA OMAR (R.A)

Elimu kwa wanawake