Joseph Temba awa bilionea wa kushitukiza Tanzania

Joseph Temba atajirika baada ya kupata almasi kubwa zaidi Tanzania

Mchimbaji Mdogo wa Madini Mkoani Shinyanga ameuza Almasi yake kwa Tsh. Bilioni 3. Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo ashuhudia.Haki miliki ya pichaWIZARA YA MADINI TANZANIA
Image captionMchimbaji Mdogo wa Madini Mkoani Shinyanga ameuza Almasi yake kwa Tsh. Bilioni 3. Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo ashuhudia.
Taifa la Tanzania limejipatia bilionea wake wa hivi karibuni baada ya mchimbaji mdogo wa madini mkoani Shinyanga kuuza almasi yake kwa takriban dola milioni moja nukta nne sawa na Tsh. Bilioni 3.
Almasi hiyo yenye karati 512 ilipatikana na mchimbaji madini mdogo Joseph Temba wiki mbili zilizopita katika eneo la Maganzo huko Shinyanga.
Bwana Temba ameishukuru Wizara ya Madini na Tume ya Madini kwa muongozo na usimamizi wa Almasi yake na muongozo wa utaratibu wa mauzo ambao uko wazi.
Ametoa wito kwa wachimbaji wadogo wezake kufuata utaratibu uliowekwa na Serikali kwani kuna faida nyingi hivyo hawana sababu ya kukwepa Masoko hayoo.
Kulingana na naibu waziri wa madini nchini humo Stanlaus Nyongo almasi hiyo ndio kubwa zaidi kuwahi kupatikana nchini humo.
Alamsi iliopatikanaHaki miliki ya pichaWIZARA YA MADINI TANZANIA
Akifichua tangazo la kupatikana kwa almasi hiyo katika mtandao wake wa Twitter bwana Nyong'o alisema kuwa serikali imejipatia shilingi milioni 238 kutokana na mauzo ya madini hayo.
Nyongo amewahimiza na kuwasisitizia wachimbaji wote na wanunuzi kote nchini kufanya shughuli hizo kwenye masoko ya madini yaliyoainishwa na kutambulika na Serikali.
Almasi ya bwana Temba ilipokuwa ikipimwaHaki miliki ya pichaWIZARA YA MADINI TANZANIA
Amempongeza bwana Joseph Temba kwa kufuata utaratibu katika mauzo yake na kwamba Serikali itaendelea kusimamia mauzo yake mpaka hatua ya mwisho.
Almasi ya waridi
Almasi ghali zaidi duniani ni ile yenye rangi ya waridi ambayo ni adimu kupatikana iliuzwa kwa dola milioni 50 kwa karati.
Almasi hiyo na ina uzito wa chini ya karati 19.
Almasi hiyo ilinunuliwa na chapa ya Harry Winston mwenye asili ya Marekani katika mnada uliofanyika Geneva.
"Karati moja iligharimu takribani dola milioni 2.6 na bei hiyo inathibitisha kuwa almasi ya rangi ya waridi ina gharama kubwa zaidi duniani", kwa mujibu wa mkuu wa nyumba ya mnada barani ulaya, Christie.
Almasi hiyo ilikadiriwa kuwa na thamani ya kati ya dola milioni 30 mpaka dola milioni 50 baada ya kuuzwa kwenye mnada ndani ya dakika tano.
Wachimba migodi wadogoHaki miliki ya pichaOLIVIA ACLAND
Almasi kubwa zaidi yenye karati 476 ilipatikana na wachimba migodi nchini Sierra Leone ikiwa ya 29 kuwai kupatikana duniani.
Hatua hiyo inajiri miezi minane baada ya almasi ya zaidi ya karati 700 kupatikana ambayo ni kabwa zaidi kuwai kupatikana nchini Sierra Leone kwa nusu karne.

Comments

Popular posts from this blog

FAIDA ZA KUOA MKE ALIEKUZIDI UMRI

HISTORIA YA KHALIFA WA PILI SAYYIDNA OMAR (R.A)

Elimu kwa wanawake