Namna ya kuandika ombi la mkopo


Namna ya kuandika ombi la Mkopo

  • Kuna dhana imejengeka miongoni mwa jamii kuwa si rahisi na kuna usumbufu mkubwa kwa wajasiriamali wadogo na wakati katika  kupata mkopo. Dhana hii sio sahihi kabisa. Itambulike kuwa mabenki yanapata pesa kupitia utoaji wa mikopo, kama yasipotoa mikopo ni dhahiri kuwa yatapata ugumu katika kujiendesha.

Kudhihirisha hilo hivi karibuni mabenki mengi yametangaza kupunguza riba za kukopesha ili tu kuwavitia watu wengi zaidi waweze kukopa.
Benki ya CRDB kwa mfano, imepunguza riba ya mikopo binafsi kutoka asilimia 22 hado asilimia 16 na imeongeza mda wa kulipa deni kutoka miaka minne hadi miaka saba. Benki ya NMB kwa  upand mwingine imepunguza riba hadi asilimia 17 na benki ya BOA imepunguza riba hadi asilimia 11. Hii inaonyesha ni kwa kiasi gani mabenki yanategemea biashara ya kukopesha ili yaweze kujipatia kipato.
Tatizo kubwa ambalo limekuwa likifanya mabenki yasitesite kukopesha ni uelewa mdogo wa wajasiriamali katika masuala ya fedha na jinsi wajasiliamali wanavyoandika maombi ya mikopo wanayoihitaji.
Kutuma maombi ya mkopo benki wakati ambapo hujajiandaa vyema na hujaandika vyema maombi yako kunapeleka taarifa kwa watoa mokopo kuwa ‘UWEZO WAKO WA KULIPA MIKOPO HIYO UTAKUWA NI MDOGO’.
Ili uweze kufanikiwa kupata mkopo ni lazima uwe umejiandaa vyema na uwe umejipangilia ipasavyo. Ni lazima ujue kwa hakika kiasi gani unahitaji, kwa nini unakihitaji na kwa namna gani utarudisha huo mkopo uliochukua. Ni muhimu uwe na uwezo wa kumshawishi mkopeshaji kuwa wewe ni mtu mzuri na kwamba unauwezo wa kurudisha mkopo kwa wakati.
Aina za Mikopo ya Biashara
Masharti ya mkopo yanatofautiana kati ya mkopeshaji na mkopeshaji, lakini kuna aina kuu mbili za mikopo; mikopo ya mda mfupi na mikopo ya mda mrefu. Mikopo ya mda mfupi ni ile ambayo inalipwa ndani ya mwaka mmoja wakati mikopo ya mda mrefu ni ile inalipwa kwa zaidi ya mwaka mmoja lakini haizidi miaka saba. Wakati mwingine mabenki hutoa mikopo ya mda mrefu inayorudhiswa ndani ya miaka hadi 25, mikopo hii ni kama vile ya nyumba na vifaa.
Jinsi ya kuandika ombi la Mkopo
Kukubaliwa kwa ombi lako la mkopo kunategemeana kwa kiasi kikubwa namna ulivyojieleza na ulivyoelezea biashara yako. Kumbuka mabenki yanahitaji sana kutoa mikopo ikiwa tu watajiridhisha kuwa mkopo huo utalipwa. Njia nzuri ya kujihakikishia kupata mkopo ni kuandika ombi la mkopo.
Ombi la Mkopo
Ombi la mkopo lililoandikwa vizuri linajumuisha vitu vifuatavyo:
  • Taarifa ya jumla
  • Taarifa ya kina ya Biashara yako
  • Taarifa za wamiliki na viongozi
  • Taarifa za soko
  • Taarifa za fedha
Taarifa za jumla zinajumuisha:-
  • Jina la biashara, jina la Wamiliki wa biashara, Namba ya Mfuko wa jamii kama unayo mfano NSSF, PPF, GEPS n.k. pia ambatanisha jina la biashara.
  • Lengo la Mkopo (Eleza kinagaubaga pesa unazokopa zitatumika kufanyia nini na kwa nini zinahitajika
  • Kiasi cha pesa unachohitaji (Pesa taslimu unazohitaji ili kufikia lengo lako)
Taarifa za Kina za biashara zijumuishe:-
  • Historia na aina ya biashara (Eleza kwa undani kuhusu aina ya biashara, umri wa biashara yako, idadi ya wafanyakazi, na mali za biashara ulizonazo)
  • Mfumo wa Uongozi (Eleza kwa undani mfumo wa kisheria wa kampuni yako)
Taarifa za Wamiliki
Andaa taarifa fupi ya kila mmiliki na taarifa za viongozi wa juu kwenye biashara yako ukielezea:-
  • Historia
  • Elimu
  • Uzoefu
  • Ujuzi
  • Mafanikio
Taarifa za soko zijumuishe:-
  • Eleza kwa kina aina ya bidhaa unazozalisha au kuuza na soko lako
  • Bainisha washindani wako na jinsi biashara yako inavyoweza kustahimili ushindani kwenye soko
  • Elezea kwa ufupi kuhusiana na aina ya wateja ulionao au unaowalenga na elezea namna biashara yako inavyokidhi mahitaji yao.
Taarifa za fedha zijumuishe:-
  • Taarifa ya mapato na matumizi kwa miaka mitatu iliyopita. Kama ndio unaanza toa taarifa za utabiri wa mapato na matumizi yako yatakavyokuwa.
  • Taarifa zako binafsi za fedha na za wamiliki wengine au viongozi wengine wa juu.
  • Aina ya Dhamana unayofikilia kuiweka.
Jinsi Mkopo wako unavyofanyiwa Tathmini
Wakati wa kupitia maombi ya mkopo, mkopeshaji anajikita zaidi kuangalia uwezo wako wa kulipa mkopo utakaopewa. Wakati mwingine huwaradhimu kutafuta taarifa zako za ulipaji wa bili mbalimbali kama vile bili za maji na umeme.
Ofisa Mkopo atakagua ombi lako kwa kuangalia vitu vifuatavyo:
  • Je umewekeza pesa zako binafsi kwenye hiyo biashara yako angalau asilimia 25 hadi asilimia 50 ya mkopo unaoomba? (Kumbuka mkopeshaji au muwekezaji hatakupatia pesa asilimia 100 kwa ajili ya biashara yako, lazima wewe mwenyewe uwe na pesa kiasi).
  • Je historia yako ya ulipaji madeni na bili mbalimbali vikoje? Je wadhamini wako wamekuelezeaje?
  • Je unauzoefu na mafunzo katika kusimamia biashara?
  • Je ombi lako la mkopo limeandikwa kwa kina na linaonyesha kinagaubaga nia yako ya kurejesha mkopo?
  • Je mzunguko wa pesa unayozalisha kila siku unatosheleza mahitaji ya kulipa mkopo kila mwezi?
 Tuishie hapa kwa leo, ITAENDELEA

Comments

Popular posts from this blog

FAIDA ZA KUOA MKE ALIEKUZIDI UMRI

HISTORIA YA KHALIFA WA PILI SAYYIDNA OMAR (R.A)

Elimu kwa wanawake