Alietelekezwa na mumewe baada ya kujifungua mapacha wanne achangiwa mlioni 32 na Wabunge

Radhia Solomon, mkazi wa Mtaa wa Chemchemi, Magomeni Mapipa jijini Dar es Salaam
aliyejifungua watoto mapacha wanne na kutelekezwa na mume wake amechangiwa na wabunge wote waliopo bungeni Sh. Milioni 32,050,000.

Wabunge wanawake watakatwa Sh50,000 na wanaume Sh100,000 kwa ajili ya kumsaidia Radhia Solomon (24) mkazi wa Kinondoni aliyejifungua watoto wanne Januari 8, 2019.
Radhia ametembelea bungeni jijini Dodoma leo Jumatatu Juni 3, 2019 na baada ya kutambulishwa na Spika Job Ndugai, alipendekeza wabunge kutoa kiasi cha fedha zao za posho leo kwa ajili ya kumchangia mwanamke huyo ombi lililokubaliwa na wawakilishi hao wa wananchi baada ya kutelekezwa na Mume wake
Kati ya fedha hizo wabunge wakiume 248 kila mmoja amechanga Sh.100,000 na wabunge wa kike 145 wamechanga Sh.50,000.
TOA MAONI YAKO KISHA #SHARE

Comments

Popular posts from this blog

FAIDA ZA KUOA MKE ALIEKUZIDI UMRI

HISTORIA YA KHALIFA WA PILI SAYYIDNA OMAR (R.A)

Elimu kwa wanawake