AFYA

Simulizi ya Lucky Ndanu, mama aliyepoteza titi kutokana na saratani

Lucky NdanuHaki miliki ya pichaLUCKY NDANU
Image captionLucky Ndanu
Lucky Ndanu mwenye umri wa miaka 31 alipatwa na saratani ya matiti alipokuwa na miaka 19.
Saratani yake ilikuwa katika kiwango cha kwanza . Ameishi bila titi moja kwa takribani miaka 12.
Bi Ndanu alianza kuhisi shida ya matiti mwaka 2007 alipokuwa katika mwaka wake wa mwisho katika taasisi moja ya kielimu nchini Kenya
Alikuwa akipata maumivu makali kila alipokuwa akivua sidiria hasa katika titi lake la upande wa kulia.
Amesema titi lake la upande wa kulia lilikuwa na mishipa iliyokuwa inajaa damu kila wakati na lilikuwa na kiwango kikubwa cha joto na tofauti kabisa na titi lake jingine.
Miaka iliyopita aligundua alikuwa na uvimbe lakini hakuutilia maanani kwani alifikiria ni jambo la kawaida katika ziwa lake.
Baada ya dalili hizo tofauti ndipo nilipoamua kwenda kumuona daktari.
Ndanu amesema daktari aliyemtembelea wakati huo alimueleza kwamba alikuwa na umri mdogo na bado anaendelea kukua. Lakini uchungu huo ulimsabishia kumtafuta daktari mwingine ili afahamu chanzo cha maumivu hayo.
Lucky NdanuHaki miliki ya pichaLUCKY NDANU
Image captionLucky Ndanu
''Nilipoenda kufanyiwa uchunguzi wa kupigwa picha daktari alisema, mimi ni mdogo siwezi kufanyiwa matibabu ya kuchomwa na miale baada ya matokea yote yalipoonyesha niko na seli za saratani.''
''Mama yangu hakuamini matokea ya uchunguzi huo na kile ninachokumbuka niliona machozi yakimwangika kutoka machoni pake, mimi nilikuwa nimechanganyikiwa na maishani sikuwa nimeskia mtu yeyote mwenye umri mdogo anaugua saratani,''Ndanu aliongeza.
''Mimi sikupitia matibabu ya kuchomwa na miale kutokana na umri wangu na saratani yangu ilikuwa katika hatua za kwanza. Katika safari yangu ya matibabu sikuweza kutoa uamuzi wa aina yoyote na kila kitu kulichofanyika kilikuwa chini ya uamuzi wa familia yangu. Hata uamuzi wa iwapo nitolewe titi langu lote au la ulifanywa na wazazi wangu."
Licha ya kutolewa titi haikuwa mwisho wa maisha yake bali alikuwa na malengo mengine ikiwemo kupata mtoto.
Miaka kadhaa baada ya upasuaji aliweza kubeba uja uzito na akajifungua bila matatizo yoyote, lakini jamaa zake walikuwa na hofu iwapo angejifungua na kumlea mtoto kwa salama.
Hofu kubwa ya ndugu ilikuwa inatokana na uhalisia kuwa mama huyo anaendelea kutumia baadhi ya dawa za kumkinga na kurejea kwa shambulio la ugonjwa huo.
Dawa hizo hazikumzuia kunyonyesha mtoto wake na alifanya hivyo kwa miezi sita bila kupa chakula kingine kama ishauriwavyo na wataalamu wa afya.
Baada ya hapo aliendelea kumnyonyesha na kumpa vyakula vingine hadi miaka miwili na mtoto sasa hivi ana afya kama watoto wengine.
Saratani ya matiti inaweza kumpata mtu yeyote wanaume au wanawake bila kuzingatia umri au jinsia.

Dalili za saratani ya matiti kwa wanaume au wanawake

  • Uvimbe katika ziwa unaokua kwa haraka
  • Chuchu ya ziwa kuingia ndani
  • Ngozi kubadilika na kuwa nyekundu
  • Titi kuongezeka kwa ukubwa
  • Chuchu kutoa damu au usaha
  • Kumea tezi kwenye kwapa
  • Maumivu katika titi.
Ni bora kuwasaidia waathirika wa saratani kwa kuwapa moyo ili waweze kufuatilia matibabu vizuri na hata kupata lishe bora.

Comments

Popular posts from this blog

FAIDA ZA KUOA MKE ALIEKUZIDI UMRI

HISTORIA YA KHALIFA WA PILI SAYYIDNA OMAR (R.A)

Elimu kwa wanawake