HISTORIA YA KHALIFA WA PILI SAYYIDNA OMAR (R.A)

HISTORIA YA KHALIFA WA PILI SAYYIDNA OMAR (R.A)
Omar bin Khatab alizaliwa mwaka 583 A.D ,asili ya familia yake inatokna na kabila LA Kikureish ..Katika ujana wake Omar alikuwa maarufu ktk upiganaji .Baadhi ya wanahistoria wa kiislam wanasema Omar (r.a) alikuwa ni miongoni mwa watu wachache waliokuwa wanajuwa kusoma na kuandika ktk Mji wa Makka kabla ya kuja Uislam .
Kazi yake kubwa ilikuwa ni biashara .Wakati Mtume s.a.w anateremshiwa wahy na kulingania Uislam Umar alikuwa ni adui mkubwa wa Uislam na Mtume (s.a.w).
Kuslimu kwa Omar bin Khattab (r.a)
Omar aliiƱgia ktk Uislam mwaka wa sita baada ya Utume.Mwaka huo viongozi wa Kikureish walieka mkutano wa kutafuta mtu atakayejitolea kumuua Mtume s.a.w .Omar alisimama na kusema yeye ni mtu sahihi wa kufanya kazi hiyo.
Wakati yuko njiani akiwa na panga alikutana na Sa'ad bin Abii Waqas .Omar alimwambia Sa'ad "nakwenda kumuu Mtume s.a.w .Baada ya majadiliano Sa'ad alisema " Kwanza unapaswa kushuhilikia familia yako na pia Dada yko na Shemeji yako wameshasilimu"
Baada ya Omar (r.a) kusia vile alibadilisha mwelekeo wake na kwenda moja kwa hadi nyumbani kwa Dada yake (Fatma).Wakati huo Omar anagonga mlango walikuwa wanafundishwa Qur'an na Khabbab (r.a).
Dada yake alishtushwa na sauti ya Omar .Baada ya Omar kuingia ndani aligundua kuwa kweli wameslimu .Hapo hapo akaenda kumshambulia Shemej yake na kumpiga .Dada yake alipotaka kuingilia kati alimshambulia na kudondoka na akawa anatoka damu ktk Uso wake .
Fatma alisema "Fanya utakavofanya sisi tumeshaingia ktk uislam na tutakufa ktk Uislam" Mara Omari alimuona Dada yake anatoka damu ktk uso wake alijiskia aibu na huruma kwasbabu alimpenda sana Dada yake .
Hapo hapo Omari alimwambia "Nifungulie Qur'an lakini Dada yake alimwambia huwezi kugusa Masahaf mpaka utie udhu " .Omar alikoga na kutia Udhu .Baada ya hapo Fatma alimfungulia Surat Twaha (20:14 )Fatma alisoma kwa sauti aya ilikuwa inaeleza .........Mimi Mungu na hakuna Mungu ...........(20:14)
Omar alisema ni kweli haya ni maneno ya Allah nipeleke kwa Muhammad s.a.w .Baada ya kuskia vile Khabbab r.a alisema dua ya Mtume s.a.w aliyoimba usiku wa jana yake imejibiwa na Allah ..Mtume s.a.w aliomba kuwa Omar bin Khattab or Omar bin Hisham mmoja wao asilimu awe muislam .
Omar (r.a) alipofika kwa Mtume s.a.w alimwambia umekuja kufanya nini Yaa Omar ?.Omar alisema "Nimekuja hapa kuslim. Maswahaba waliokuwepo kwa pamoja walisema Allah Akbar .
Kuslimu kwa Omar kuliwahuzunisha na kuwasononesha Makurwish wa Makkah hii ni kutokana nguvu na kukubalika ktk mji wa Makkah
Abdallah bin Masuud alikuwepo pale na akasrma " kuislimu kwa Omar ni Ushindi kwa Uislam " .Na ni kweli kabisa baada ya Omar kuingia ktk Uislam Uislam ukipata nguvu kwsbb watu wengi walislim baada ya kufahamu ukweli juu ya Uislam .
Itaendelea In Shaa Allah

Comments

Popular posts from this blog

FAIDA ZA KUOA MKE ALIEKUZIDI UMRI

Elimu kwa wanawake