Wahubiri wanaopata utajiri kutoka kwa watu masikini

Wahubiri wanaopata utajiri kutoka kwa Wamarekani masikini

Larry na Darcy FardetteHaki miliki ya pichaJOSEPH DE SCIOSE
Image captionLarry na Darcy Fardette walitoa pesa nyingi kwa wahubiri mbali mbali
Mhubiri anayefikisha ujumbe wake kwa njia ya Televisheni Todd Coontz amekuwa na mtindo wa kuvaa mavazi ya kupendezahuvalia sutina kutoa Biblia yake huku akiwataka watazamaji wake kutoa ahadi za kiasi fulani cha pesa. "Usichelewe, usichelewe," huwaagiza watazamaji wake akiwa mtulivu lakini kwa kauli ya kuwalazimisha.
Husikika kama jambo rahisi, , lakini Coontz anawafahamu vizuri watazamaji wake. Hutoa mahubiri yake katika Televisheni ya Kikristo, mara nyingi wakati wa usiku, na kuwavutia watazamaji wanaokabiliwa na matatizo ya kifedha na ambao wanataka mabadiliko.
"Nafahamu sheria zinazolinda bima yenu , hisa, riba na yote yanayohusiana na soko la kibiashara la Wall Street," aliwahi kusema wakati mmoja huku akitazama moja kwa moja kwenye kamera ya televisheni. "Nimeitwa na Mungu … kama mtu wa kuwasilisha pesa."
Muhimu, huelezea pesa kama "mbegu" - mbegu ya $273, mbegu ya $333 na mbegu ya "mabadiliko", kulingana na matangazo . Kama watazamaji "wanapanda " moja, kiasi hicho kinawarudia mara dufu. Ni uwekezaji katika imani zao na hali zao ya baadae.
Short presentational grey line
Mnamo mwaka 2011, mmoja wa watazamajiwaliokuwa wakitaka kupata mabadiliko ya kifedha alikuwa ni Larry Fardette, ambaye alikuwa akiishi California.
Larry aliwatazama wahubiri wengi kwenye televisheni ambao walihusisha utajiri na mahubiri . Lakini aligundua kuwa Coontz alikuwa na mvuto wa kipekee . Alitoa hakikisho la kupata faida haraka .
Alionekana kama mtumishi mwenye matokeo.
Na Larry alihitaji matokeo ya haraka.
familia ya Fardetteilikuwa inapitia kipindi kigumu . Binti yake Larry alikuw amgonjwa sana na alikuwa na matatizo yake binafsi ya kiafya . Biashara yake ya ujenzi haikuwa inafanya vizuri na baya zaidi basi lake dogo lilikuwa limeharibika katika wiki hiyo hiyo . Wakati jihrani yake alipompatia msaada wa $600 kwa ajili ya kutengeneza basi lake , aliweza akuwa ameazimia kulipia gharama za matengenezo ya gari , lakini akafikiria hotuba ya muhubiri Coontz ya kuvutia
Akawaza labda angewekeza sehemu ya pesa hizo kama "mbegu"?
Alituma hundi mbili moja ya $273 na nyingine ya $333, kama alivyoagizwa. Kisha akasubiri muujiza.
Larry amekuja kugundua kuwa hapakuwa na msingi wa ahadi za Coontz na kwamba ukitoa pesa utapata maradufu , lakini wakati huo mahubiri ya kuvutia yalimpatia matumaini. Hakuwa na njia nyingine.
Todd CoontzHaki miliki ya pichaTHE WORD NETWORK / YOUTUBE
Image captionTodd Coontz anadai kuwa mtaalamu wa masuala ya kifedha
Wahubiri wa televisheni hawazungumziwi sana siku hizi kama ilivyokuwa katika miaka ya 1980 na 1990, wakati wengi walipata umaarufu na utajiri kupitia vituo vya televisheni vilivyoibuka na kushamiri.
Lakini hawajaenda popote. Hata baada ya uchunguzi kadhaa kufichua hila zao mara kwa mara wamekuwa wakiendelea na shughuli zao. Baadhi wamekuwa hata matajiri zaidi .
Wengi wamepeleka maombi yao kwenye mitandao ya pesa kijamii.
Baadhi ya wale wanaoendelea kuomba pesa wamegeuka na kuwa wahubiri wa injili ya mafanikio na hivyo kuwaambia wafuasi wao kuwa utajiri wao ni wa Mungu na hawana usemi juu ya utajiri wao.
Waumini huambiwa wadhihirishe imani zao kwa kutoa pesa ambazo wanafikiri kuwa zitaongezeka mara nyingi - ima kwa njia ya utajiri au kupitia uponyaji.
Larry Fardette at home in Cullman, AlabamaHaki miliki ya pichaJOSEPH DE SCIOSE
"Maisha si rahisi lakini tumebarikiwa ," anasema Larry . "Tunachakula kwenye friji, tuna paka wawili wanaotupenda, mke wangu ana kibarua na ninapata msaada wa walemavu."
Baada ya kuamua "kufuata njia ya kristo", alikuwa mtazamaji sugu wa televisheni za kidini na hasa "praisathons" - matukio ya kuchangisha yenye wageni wazungumzaji wengi.
Akawa katika dunia yake, kulingana na maelezo yake mwenyewe , "shabiki " wa wahubiri. Hakuwa tu shabiki wa kawaida,alihisi kana kwamba anawafahamu.
Na wengi wa wahubiri walikuwa na laini za simu na pale walipoomba pesa wafuasi wao, Larry alifurahia kuchangia, hata kama hakuwa na pesa nyingi za kutoa.
Alifurahia kwamba pesa zake zililkuwa muhimu kwa miradi ya nyumbani na nje ya nchi, na alitumaini kwamba kama angejikuta katika hali mbaya basi angesaidiwa pia.
Picha kwenye ukuta wa nyumba ya Larry Fardette ya Cullman, AlabamaHaki miliki ya pichaJOSEPH DE SCIOSE
Mnamo 2013, muda uliwadia.
Hali ya afya ya binti yake ambayo ilikuwa mbaya kwa muda mrefu ilizidi kuwa mbaya zaidi. Larry alimuahidi kumsaidia kifedha lakini "mbegu " yake ilikuwa imenyauka .
Aliyaandikia makanisa kadhaa barua yake ya kurasa tano aliyokuwa akiyachangia pesa kwa miaka akielezea hali mbaya ya binti yake akiyaomba msaada.
"Tulikuwa waaminifu kwa makanisa haya. Walituita washirika, marafiki, wanafamilia " anaeleza sasa . "Tulifikiri wangetusaidia ."
Majibu yalipatikana, baadhi yakijibiwa mara moja kwa barua pepe, mengine yalikuja kwa njia ya posta lakini maombi yote yalikataliwa.
"Walisema mambo kama, ' kanuni za kanisa zinatuzuwia kukusaidia," amesema.
Anakumbuka moja ya majibu kutoka kwa mhubiri mmoja wa kanisa ambalo lilikuwa limejinadi kuwa linatoa msaada wa ufadhili wa matibabu nchini Marekani.
"Kwa sauti ya kiburi, alichukua simu kisha akavuta pumzi na kusema: 'Unajua tunapokea simu sita au saba za aina hii kwa wiki na kama tukikusaidia wewe itabidi tumsaidie kila mtu.
Mnamo mwaka 2013, mmoja wa majirani wa Todd Coontz aliipigia simu televisheni ya eneo hilo kulalamikia kuwa amechukua eneo kubwa la kuegesha magari nje ya makazi yake ya kifahari South Carolina katika jengo la ghorofa.
Wakati ripoti kuhusu WSOC -TV ya Coontz ilipotangazwa , iliibua hisia zaidi ya mzozo wa kuegesha magari , ikielezea kwa kina utajiri wake wa kibinafsi na kuonyesha kushuku uhalali wa njama zake za kuchangisha pesa za misaada.
Todd CoontzHaki miliki ya pichaWSOCTV.COM
Image captionMuhubiri Todd Coontz akielekea mahakamani
Todd Coontz hayuko sawa na baadhi ya wahubiri wa mafanikio ya utajiri . Hana kanisa kubwa, kiwanja chake cha ndege au hata ndege yake aina ya jet. Huhubiri katika matukio ya watu wengine ya moja kwa moja , badala yake wahubiri wengine huhubiri chini ya nembo la jina.
Lakini mtindo wa maisha yake ni wa ghali mno. Amekwishaweka picha zake kwenye ukurasa wa Facebook kuhusu namna anavyoishi katika hoteli ya kifahari ya Rodeo Drive iliyopo eneo la kifahari la Beverly Hills wanakoishi nyota wa Filamu za Hollywood.
Hutumia maelfu ya pesa kununua vito vya thamani vilivyotengenezwa kwa Almasi pamoja na vipuli vya thamani ya juu.
Pia ana mali nyingi miongoni mwake magari ya kifahari kama vile BMW tatu, Ferraris mbili, Maserati moja na Land Rover, pamoja na mtumwi wa mwendo kasi.
Alifanyiwa uchunguzi wa miaka minne na wakati wa uchunguzi huo waendesha mashtaka walibaini makosa mengi na kuamuru kuwa Coontz amekuwa akificha kuripoti nyingi kati ya mali zake na madai ya gharama za mali za watu anazozichukua.
Januari 26 2019, Coontz alihukumiwa kifungo cha miaka mitano jela kwa kushindwa kulipa kodi na kusaidia kujaza fomu gushi za malipo ya ushuru .
Aliagizwa kulipa faini ya $755,669.
Alifika gerezani mapema mwezi Aprili lakini aliachiliwa huru na majaji, huku akisubiri kesi yake ya rufaa.
Coontz hakujibu swali la BBC' kuhusiana na kile anachosema juu ya kesi dhidi yake, lakini awali alikana kuhusika na kosa lolote lile, katika tovuti yake pia alidai kuwa alitoa pesa zaidi ya dola milioni 1 za msaada.
Akaunti yake ya mtandao wa Twitter bado inatuma ujumbe kila siku (bila kutaja hukumu yake ya jela ) na sasa anahubiri kutoka kwenye makazi yake ya kifahari kwa kutumia App.
"Unaniita kupanda mbegu yako ya $219 leo?" lilikuwa ni jibu lake la moja kwa moja wakati BBC ilipoita namba yake maalum ya mahubiri. " Sio wengi leo, lakini tuko wengi tunaopokea simu ," alisema mmoja wa wahudumu wake wa kupokea simu.
Haikuwa wazi iwapo huduma hiyo ya kupokea simu ilikuwa ni ya Rockwealth au hata makanisa mengine pia.
Cullman, AlabamaHaki miliki ya pichaJOSEPH DE SCIOSE
Image captionCullman, Alabama, mji ambao bwana Larry anaishi kwa sasa
"Panga uwekezaji wako wa muda wako, kipaji, pesa ndani ya jamii yako na utawapata watu wanaohitaji msaada ," alisema Larry, na kuongeza kuwa anawafahamamu binafsi majirani zake wachungaji.
Mabinti zao wanaishi, lakini baada ya Larry kushindwa kulipia matibabu ya binti yake ukazuka uhasama baina yao na sasa hawaongei.
Larry na mkewe wanasema wanataka kuwashirikisha watu na hadithi yao ili kuwafanya wafikirie mara mbili kuhusu ni wapi pesa zao zinakwenda.
"Tulijifunza kwa njia ngumu. Hii ni biashara ya kutengeneza pesa," alisema larry kwa msisitizo. .

Comments

Popular posts from this blog

FAIDA ZA KUOA MKE ALIEKUZIDI UMRI

HISTORIA YA KHALIFA WA PILI SAYYIDNA OMAR (R.A)

Elimu kwa wanawake