NI S 400 AU KUANGUKA KWA MAREKANI?

i S 400 au ni Kuanguka kwa mhimili wa Marekani ?

Prof. Dr. Kudret BÜLBÜL’ün  mkuu wa kitivo cha elimu ya siasa chuo kikuu cha Ankara Yıldırım Beyazıt anafafanua kuhusiana na nidhamu za ulimwengu

Ni S 400 au ni Kuanguka kwa mhimili wa Marekani ?
Vipindi fulani katika historia huwa ni muda wa kuanzisha nidhamu, Nidhamu inayoanzishwa katika vipindi hivi huelekea mpaka katika mazingira ya mtafaruku au kutoelewana. Nidhamu ya “West phalia” iliyomaliza vita vya miaka 30 barani Ulaya, Nidhamu ya vita baridi iliyoanzishwa na mkutano wa Yalta baada ya kumalizika vita kuu ya 2 ya dunia ni katika nidhamu za kwanza za kidunia zinazoweza kukumbukwa. Katika mkutano wa Yalta aliyekuwa waziri mkuu wa Uingereza Winston Churchill, Rais wa Marekani Franklin Roosevelt pamoja na aliyekuwa Rais wa muunganiko wa dola za kisovieti Josef Stalin, mwaka 1945 walikutana katika kijiji kidogo cha Krimea eneo la Yalta na kuweka misingi ya nidhamu ya vita baridi ambayo mpaka hii leo hakuna nidhamu nyingine iliyochukua nafasi ya nidhamu hii ya vita baridi.
Prof. Dr. Kudret BÜLBÜL’ün  mkuu wa kitivo cha elimu ya siasa chuo kikuu cha Ankara Yıldırım Beyazıt anafafanua kuhusiana na mada hii...

Utafutaji wa nidhamu mpya ya kilimwengu
Tunapozungumzia “nidhamu ya kilimwengu” siyo lazima nidhamu hiyo iwe katika msisingi ya haki, maridhiano au manufaa mengine ya pamoja ya kiutu. Kutafuta haki ya kiulimwengu ni mada tofauti, ni hitajio na tafutwa tofauti. Kwa nidhamu ya kilimwengu inamaanisha mfumo ambao utafanya kazi dunia nzima ambao watendaji wanatambuliwa na pande tofuati zinakubaliana iwe kwa maridhiano au kwa kulazimishwa. Hauhitajiki kujengwa katika msingi ya kiuadilifu, na mara nyingi haipo kiuadilifu. Ni nidhamu ambazo nafasi itakayochukuliwa inafahamika na hivyo basi matokeo yanaweza kutabiriwa..
Utu umeimaliza  nidhamu ya vita baridi katika karne ya 21 lakini vile hakuna nidhamu mpya iliyoanzishwa imeingia hali ya kulegalega. Nidhamu ya vita baridi baina ya mataifa ya magharibi na mashariki iliyotokana na mikataba ya NATO na WARSAW ilimalizika mara baada ya muungano wa kisovieti kuparanganyika.
Katika hali iliyopo inaweza kusemwa ncha mbili za nidhamu ya vita baridi imeendelea kuwepo katika hali ya mihimili minne.
Mhimili wa Marekani: Marekani yenyewe ikijichukulia kama kitovu inajaribu kuendeleza ubeberu wa Marekani. Inayafanya haya kwa  kuacha pembeni sera zisizo za kutumia nguvu ambazo zilijaribu kuwavutia watu kama vile “ndoto za Marekani” “american dream” na kuanza kutumia sera za kimabavu zinazolenga moja kwa moja maslahi ya nchi hio.Hivi sasa Marekani haitegemewi kurudi iongoze tena ushindani wa kiulimwengu kwa kutumia ajenda chanya ya kiuzalishaji. Ni kwa sababu hiyo Marekani imekuwa ikitumia sera ambazo zinazuia mataifa mengine kuongoza katika ushindani wa kiulimwengu.Katika muktadha huu Marekani ambayo hapo mwanzo ndiyo iliyokuwa bingwa wa utandawazi hivi sasa sera ambazo ni kinyume na utandwazi ndio zimekuwa uti wa mgongo wa taifa hilo.
Mhimili wa Urusi : Baada ya kuvunjika kwa Muungano wa kisoviet “USSR”, Urusi inafanya juhudi za kujikusanya na kusimama upya. Kwa vile Urusi haikuwahi hata mara moja kuwa kitovu cha kivutio katika ngazi ya kidunia kazi hii ya kujikusanya na kusimama upya inafanywa zaidi kijeshi na kwa kutumia sera nyingine za kimabavu.
Mhimili wa Uchina: Uchina imejitokeaza kuwa nguvu kubwa ya kiuchumi kwa ufanisi mkubwa lakini bado haijawa nguvu kubwa kwa upande wa kijeshi na kisiasa. Wakati wadau ukianza na Marekani ikionyesha wazi wazi rasilimali zake za kijeshi na kisiasa kwa upande wa Uchina mpaka hivi sasa imeamua kuonyesa ubavu wake kwa kutumia nguvu za kiuchumi na kiteknolojia. Hata kama ingeweza sana kutawala kisiasa lakini tunaona inakwepa kuchukua nafasi ya kisiasa kwa sasa. Mfano inaonekana ni jinsi gani Marekani inaiunga mkono India katika hali ya juu kabisa dhidi ya Uchina, Lakini Uchina katika suala la Kashmiri haijaonyesha wazi kuwa dhidi ya India.
Hitajio la muhimili ambao kitovu chake ni uadilifu
Muhimili wa nne ni uadilifu wa kidunia, kwa bahati mbaya muhimili wa aina hiyo haupo mpaka hivi sasa. Nje ya wadau wa hapo juu ambao vitovu vyao ni maslahi yao, hitajio na utafutaji wa uadilifu kwa ngazi ya kidunia unajidhihirisha.
Mhimili wa uadilufu wa kidunia sio tu utaendesha siasa za kidunia kwa misingi bali pia itatoa msawazo kwa mihimili mingine iliyo kimaslahi. Na hilo ni suala linalohitajika kwa haraka sana.
Umoja wa Ulaya ulioanzishwa katika karne ya 20 umejidhihirisha kwamba umeshindwa kuwa mdau katika ngazi ya kidunia. Katika karne ya 21 Umoja wa Ulaya bado unalegalega. Pamoja na hayo Umoja wa Ulaya kama Umoja na sio nchi moja moja unaweza kusemwa umeonyesha baadhi ya juhudi katika kutafuta uadilifu wa kidunia.
Uturuki nayo imekuwa mstari wa mbele katika kutafuta mhimili wa kidunia uliosimama kwa misingi ya uadilifu, Kiufupi hilo linaweza  kuonekana kupitia sera zake za kikanda au kupitia miito  na juhudi zake  kama “Dunia ni kubwa kuliko tano”. Pamoja na hayo haiwezi kusemwa kwamba kuna mataifa ya kutosha ambayo yanapaza sauti zao na kufanya juhudi ya kutafuta mhimili wa kidunia ambao kitovu chake ni uadilifu.
Wadau wa mhimili ambao msingi wake ni uadilifu, amani na misingi ya kimaadili ili waweze kuonyesha uwepo wao na kufanya uwepo wao ujulikane ni budi kushirikana na kuwa siasa zilizo hai zaidi.
Wiki ijayo tutaendelea kujadili mgogoro baina ya Uturuki na Marekani kuhusiana na mfumo wa makombora wa ulinzi wa anga S 400. Lakini kwa sasa itoshe tu kusema kwamba kiini cha mgogoro huu sio mfumo wa S 400 kama inavyoandikwa na kusisitizwa na waandishi wa magharibi na kimagharibi kinyume chake chanzo cha tatizo hili sio Uturuki bali zaidi ni mabadiliko ya vipaumbele vya kidunia vya magharibi na haswa haswa Marekani na jinsi inavyosimama. Ifahamike kwamba kama vipaumbele vya Marekani vya kipindi cha vita baridi vilivyo tofauti kabisa na visivyozingatia maslahi ya nchi nyingine visipobadilika basi migogoro kama ya S 400 na mengine inayofanana itaendelea kuwepo.

  Ufafanuzi wa Prof. Dr. Kudret BÜLBÜL mkuu wa kitivo cha elimu ya siasa chuo kikuu cha   Ankara Yıldırım Beyazıt

Tagi: Nidhamu , Uturuki , Urusi , Uchina , Marekani

Comments

Popular posts from this blog

FAIDA ZA KUOA MKE ALIEKUZIDI UMRI

HISTORIA YA KHALIFA WA PILI SAYYIDNA OMAR (R.A)

Elimu kwa wanawake