MAPISHI

 · 
 · 
Vipimo
Unga 5 Vikombe
Tui la Nazi zito vugu vugu 1 ¼ kikombe
Sukari 3/4 kikombe cha chai
Samli iliyoyayushwa au mafuta 3 vijiko vya Supu
Hamirah 2 Vijiko vya Supu
Hiliki 1/2 Kijiko cha chai
Mafuta ya kukaangia

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
1. Ndani ya kibakuli kidogo, mimina hamira na na vijiko viwili vya kulia vya tui. Weka kando mpaka hamira ianze kufura, kama dakika 5-10.
2. Pasha samli moto
3. Ndani ya bakuli kubwa au sinia, changanya unga, sukari, iliki na samli ikiwa bado moto moto.
4. Mimina hamira ndani ya mchanganyiko wa unga. Changanya na ukande huku ukitumia lile tui la nazi. Tui likipungua unaweza ukaongeza maziwa. Kanda unga mpaka uwe laini.
5. Kata madonge *12 au 15 uyaweke kwenye baraza iliyonyunyiziwa unga na uyafunike ili yapate kufura na yasikauke.
*Ukipenda maandazi manene fanya madonge 12. Ukipenda mepesi fanya madonge 15
7. Pasha mafuta moto kwenye karai. Maandazi yako tayari kukaangwa sasa.
8. Kaanga maandazi kwenye mafuta ya moto. Upande mmoja ukifura na kuwa rangi nzuri geuza upande wa pili. Endelea nama hii mpaka maandazi yote yawe tayari.
TAFADHALI #SHARE NA MARAFIKI WASOME.

Comments

Popular posts from this blog

FAIDA ZA KUOA MKE ALIEKUZIDI UMRI

HISTORIA YA KHALIFA WA PILI SAYYIDNA OMAR (R.A)

Elimu kwa wanawake