BURDAN:HARMONIZE AWAZAWADIA WAZAZI WAKE MAGARI MAWILI KILA MMOJA LEKE

HARMONIZE AWAZAWADIA WAZAZI WAKE MAGARI MAWILI | BABA LAKE NA MAMA LAKE
Mwanamuziki wa bongo fleva kutoka lebo ya WCB Harmonize amewazawadia wazazi wake zawadi ya magari mawili mapya aina ya Harrier New Model ambapo kila mmoja amempatia gari lake.
Kupitia insta story ya ukurasa wake instagram Harmonize amepakia kipande cha video akiwakabidhi magari hayo Harmonize akiwa na mpenzi wake Sarah walikua na furaha kubwa huku wazazi wa Harmonize akipewa funguo na kila mmoja kufungua gari lake.
Gari aina ya Harrier new model huuzwa kwa bei ya kati ya Tsh milioni 20 mpaka 30.
Hili ni somo tosha ya kuwa tunapofanikiwa hata kwa kidogo au kikubwa tusiwasahau wazazi au walezi wetu kwani wao ndiyo daraja la wewe kufika katika hayo mafanikio unayoyapata ili Baraka tele ziendelee kumiminika kwako.
Asante sana kwa kusoma.
Unaweza tazama picha hapa.

Comments

Popular posts from this blog

FAIDA ZA KUOA MKE ALIEKUZIDI UMRI

HISTORIA YA KHALIFA WA PILI SAYYIDNA OMAR (R.A)

Elimu kwa wanawake