Namna ya Kuandaa Mchanganuo wa biashara
Maana ya na umuhimu wa mchanganuo Mchanganuo wa biashara ni andiko ambalo linaweka bayana malengo na madhumuni ya biashara na namna yatakavyofikiwa. Ni mpangilio maalum wa kuongoza utekelezaji wa kufanikisha lengo la biashara. Kuandaa mpango wa biashara ni muhimu kwa mafanikio ya biashara yoyote. Mchanganuo wa biashara hutoa dira na kusaidia kuongoza uendeshaji wa biashara. Mara nyingi ni sharti mojawapo katika kuomba mkopo. Mpango wa biashara ulioandaliwa vizuri utatoa majibu ya maswali mbali mbali kama vile nini madhumuni ya biashara yako, Utamwuzia nani/akina nani? Ni yapi malengo yako ya mwisho? Utagharimia vipi biashara yako? na mengine mengi Mpango wako wa biashara utakusaidia kutafakari mwelekeo wa kampuni yako na namna ambavyo itakabiliana na changamoto mbalimbali ili iwe endelevu. Vipengele muhimu vya Mchanganuo wa Biashara Vipengele muhimu vya Mchanganuo wa Biashara ni kama vifuatavyo:- 1. Ufupisho Kipengele hiki huandikwa mwishoni. Andika katika kipengele hiki mambo...
Comments
Post a Comment