AAMUA KUJIOA MWENYEWE

BINTI MMOJA ALIVYOWASHANGAZA WENGI BAADA YA KUAMUA KUJIOA
Binti mmoja wa nchini Kenya amewashangaza wengi baada ya kuamua kujioa kupitia harusi iliyofana sana.
Amini usiamini, Georgina Wambui, alifanya harusi ya kukata na shoka ambapo alijioa mwenyewe na kuiacha familia yake vinywa wazi.
Dada huyo mwenye umri wa miaka 33 aliliambia jarida la TUKO kwamba alikuwa na mpenzi siku za nyuma lakini penzi lao likasambaratika na akaanza kuishi bila ya mwanaume.
Mambo yalizidi kuharibika 2014 baada ya kuhusika katika ajali iliyomwacha na majeraha mabaya ambayo hadi leo yamemfanya kuwa mlemavu.
"Baada ya ajali, niliwapoteza marafiki wengi ambao walikuwa karibu na mimi. Jambo hilo lilinibadilisha sana na kunipa nguvu. Niligundua si marafiki wote wa kudumu," alisema katika mahojiano na jarida hilo.
Mnamo Juni 1, 2018 familia yake ilishangaa sana wakati aliposherekea siku ya kuzaliwa kwake kwa kujinunulia pete na kuwaeleza marafiki kuhusu mapango wa kutaka kujioa mwaka uliofuata.
Ahadi hiyo ilitimia Juni 1, mwaka huu alipofanya harusi.
"Niliamua kufanya hivyo ili kuiridhisha nafsi yangu na ila si eti siamini kuna mapenzi. Nashabikia ndoa pia lakini nimefanya nipendalo na wala si kulingana na vile jamii inataka," alisema.
Wambui aliongeza kuwa alikuwa na matumaini mengi ya kuolewa lakini hakuna mtu aliyejitokeza kumchumbia.
"Unaweza kuwa umeamua kusubiri, lakini utasubiri mtu maisha yako yote? Nilitaka sana nimpate jamaa anioe lakini sasa hakuna aliyejitokeza," aliongeza kusema.
Licha ya kujioa, dada huyo alisema ana matumaini ya kupata mtoto.
"Baada ya kufanya harusi, sasa nipanga kumpata mtoto ... hapo ndipo ninapoelekea," alisema.
=> Usisahau Kulike, Kucomment na Kushare na Marafiki.

Comments

Popular posts from this blog

FAIDA ZA KUOA MKE ALIEKUZIDI UMRI

HISTORIA YA KHALIFA WA PILI SAYYIDNA OMAR (R.A)

Elimu kwa wanawake