UHASAMA KATI YA IRANI NA SAUDIA NA UWEZO WA KIJESHI NANI ZAIDI

Je uhasama kati ya Saudia na Iran unasababishwa na nini?

Kiongozi wa dini nchini Iran Ayatollah Ali Khamenei (kushoto) na Mwanamfalme wa Saudia Mohammed bin SalmanHaki miliki ya pichaREUTERS/EPA
Image captionKiongozi wa dini nchini Iran Ayatollah Ali Khamenei (kushoto) na Mwanamfalme wa Saudia Mohammed bin Salman
Saudi Arabia na Iran wamekuwa wapinzani wakuu na hii ndio sababu.

Kwa nini Saudia na Iran hawapatani?

Saudi Arabia na Iran - majirani wawili wenye uwezo mkubwa wamekuwa wakizozana kila mmoja akitaka kuonekana mwenye uwezo katika eneo la mashariki ya kati.
Uhasama huo wa muongo mmoja sasa kati ya mataifa hayo mawili unasababishwa na tofauti ya kidini. Mataifa hayo mawili yanafuata madhehebu mawili ya kidini ya Kiislamu.
Iran ina Waislamu wengi wa madhehebu ya Kishia huku Saudia ikijiona kuwa ndio taifa la madhehebu ya Kisunni linaloongoza kwa uwezo.
Ramani inayoonyesha watu wa madhehebu ya Sunni waliovyoenea mashariki ya kati
Image captionRamani inayoonyesha watu wa madhehebu ya Sunni waliovyoenea mashariki ya kati
Presentational white space
Ukweli huu wa kidini unadhihirika katika ramani ya eneo la ,mashariki ya kati , ambapo mataifa yenye idadi kubwa ya wafuasi wa Sunni au Shia , wengine wao wakidaiwa kutegemea Iran ama Saudia kwa msaada ama muongozo.
Kihistoria Saudia , ambalo ni taifa la ufalme na chimbuko la dini ya kiislamu , linajiona kuwa taifa kubwa la ulimwengu wa Waislamu.
Hata hivyo fikra hiyo ilipingwa mwaka 1979 na taifa la Iran ambalo liliunda jimbo jipya linaloongozwa kwa jina la Mungu ambalo lilikuwa na lengo la kupanua mfumo huo katika mataifa mengine.
Ramani inayoonyesha jinsi wafuasi wa madhehebu ya Shia walioenea katika eneo la mashariki ya kati
Image captionRamani inayoonyesha jinsi wafuasi wa madhehebu ya Shia walioenea katika eneo la mashariki ya kati
Presentational white space
Katika kipindi cha miaka 15 iliyopita tofauti kati ya Saudia na Iran imenolewa na baadhi ya msururu wa maswala kadhaa.
Uvamizi wa Marekani nchini Iraq uliosababisha kuondolewa madarakani kwa Sadam Hussein , Mwarabu wa madheheu ya Kisunni ambaye alikuwa mwandani mkuu wa Iran.
Hatua hiyo ilikuwa pigo kubwa kwa Iran kwa kuwa ilipunguza ushawishi wa Iran katika taifa la Irqn ambao ulikuwa unazidi kuongezeka.
Graphic
Presentational white space
Mwaka 2011 mgogoro uliotokea katika ulimwengu wa Waarabu ulisababisha ukosefu wa uthabiti wa kisiasa katika eneo lote la mashariki ya kati.
Iran na Saudia walitumia ghasia hizo ili kupanua ushawishi wao hususan nchini Syria, Bahrain na Yemen hatua iliongeza uhasama baina yao.
Wakosaji wa Iran wanasema kuwa taifa hilo linalenga kujiimarisha pamoja na wandani wake katika eneo hilo ili kudhibiti ukanda wa ardhi ulioenea kutoka Iran hadi Mediterranean.

Kwanini uhasama huo umeongezeka katika siku za hivi karibuni

Uhasama huo wa kimkakati unazidi kuongezeka kwa kuwa Iran kwa kiwango kikubwa imekuwa ikiungwa mkono na mataifa ya eneo hilo.
Nchini Syria, hatua ya Iran na Urusi kumuunga mkono rais Bashar Al -Assad imevivuruga vikosi vya kijeshi vinavyoungwa mkono na Saudia.
Saudia inajaribu kwa hali na mali kuzuia ushawishi wa Iran unaoongezeka na hatua za kijeshi za mwanamfalme Mohammed bin Salman zinazidi kusababisha mvutano wa kikanda.
Mwanamfalme wa Saudia Mohamed Bin Salman
Anapigana vita dhidi ya waasi wa taifa jirani lililopo upande wa kusini la Yemen , kama njia ya kukabiliana na ushawishi wa Iran , lakini baada ya kipindi cha miaka mitatu hatua hiyo inaonekana kuwa gharama kubwa kwake.
Wakati huohuo nchini Lebanon wachunguzi wengi wanaamini kwamba Saudia ilimshinikiza waziri mkuu wa taifa hilo kujiuzulu ili kuweza kuiyumbisha nchi ambayo washirika wa Iran wapiganaji wa madhehebu ya shia Hezbollah wanaongoza na wanadhibiti jeshi lenye uwezo mkubwa.
Pia kuna shinikizo kutoka nje. Saudia imekuwa ikiungwa mkono na utawala wa rais Trump huku Israel ambayo inaiona Iran kama tisho pia nayo inaunga mkono juhudi za Saudia kuidhibiti nchi hiyo.
Abdul Fattah al-Sisi (kushoto), Salman bin Adbulaziz (katikati) na rais Donald Trump wakiweka mikono yao katika dunia iliongara mjini , Riyadh (21/05/17)Haki miliki ya pichaEPA
Taifa hilo la Kiyahudi lina hofu kubwa kuhusu wapiganaji wa Syria wanaoungwa mkono na Iran kuwa karibu na mpaka wake.
Israel na Saudia ndio mataifa mawili yanayopinga makubaliano ya mpango wa Kinyuklia wa Iran yakidai kwamba makubaliano hayo hayana uwezo wa kulizuia taifa hilo kuunda bomu la kinyuklia.

Washirika wao wa kieneo ni akina nani?

Kwa marefu na mapana ramani ya kimkakati ya eneo la mashariki ya kati inadhihirisha tofauti kubwa iliopo kati ya madhehebu ya Sunni na yale ya Kishia.
Ramani inayoonyesha mataifa washirika
Presentational white space
Katika kambi ya Saudia ni washirika wengine wa madhehebu ya Kisuni katika eneo la Ghuba - UAE, Kuwait na Bahrain, pamoja na Misri na Jordan.
Katika kambi ya Iran ni serikali ya Syria ambayo imekuwa ikiungwa mkono na Iran, na maeneo ambayo wapiganaji wa Kishia wapo ikiwemo wapiganaji wa Lebanon wa Hezbollah, ambao wamechukua jukumu kubwa katika kukabiliana na waasi wa Kisuni.
Madhebu ya Kishia ndio mengi katika serikali ya Iraq na ni mshirika mkuu wa Iran, licha ya kwamba taifa hilo pia lina ushirikiano mkubwa na Marekani ambayo ndio msaidizi wake mkuu katika vita dhidi ya wapiganaji wa Islamic State.

Je uhasama huo kati ya Saudia na Iran unaendelezwa vipi?

Uhasama huo ni sawa na vita baridi , kama vile vilivyotokea kati ya Marekani na Urusi katika kipindi cha miaka mingi.
Iran na Saudia hawapigani moja kwa moja lakini wanapigana kupitia washirika wao katika eneo hilo.
Syria ni mojawapo ya mifano mikuu huku Yemen- Saudia imeishutumu Iran kwa kusambaza makombora ya masafa marefu yanayorushwa katika maeneo yanayokaliwa nataifa hilo na waasi wa Houthi- tukio lililoongeza vita vya maneno kati ya mataifa hayo mawili.
Waasi wa Houthi mjini Sanaa (file photo)Haki miliki ya pichaREUTERS
Image captionYemeni ni mojawapo ya maeneo ya mapambano kati ya Iran na Saudia
Lakini licha ya kuhangaishwa nchini Yemen na kupata pigo nchini Syria , Saudia inaonekana ikielekea Lebanon kuendeleza vita vyake katika taifa hilo.
Mgogoro nchini Lebanon huenda ukaishirikisha Israel dhidi ya kundi la Hezbollah na hatua hiyo huenda ikasababisha vita vya tatu kati ya Israel na Lebanon na kuwa vibaya zaidi ya vile vita vyao vya awali.
Wachanganuzi wa Saudia wanatathmini kwamba huenda mwanamfalme wa Saudia anapanga njama ya kuzua vita dhidi ya Israel na Hezbollah ili kuliangamiza kundi hilo kupitia njia hiyo.
Je tunaelekea katika vita vya moja kwa moja kati ya Saudia na Iran?
Kufikia sasa Tehran na Riyadh wamepigana kupitia washirika wao.
Mataifa yote mawili hayana mpango wa kukabiliana moja kwa moja lakini shambulio moja la roketi kutoka Yemeni ilioanguka katika mji mkuu wa Saudia linaweza kuzua vita.
Eneo moja la wazi ambapo wanaweza kugombana moja kwa moja ni katika maji ya Ghuba ambapo mataifa hayo yanagawana mpaka.
Lakini katika eneo hilo vita vyovyote vinaweza kusababisha mzozo mkubwa.
Kwa Marekani na mataifa mengine yalio na uwezo mkubwa kutoka eneo la magharibi , uhuru wa kupita katika maji hayo ya Ghuba ni muhimu na mgogoro wowote ambao unaweza kufunga mkondo huo wa bahari ulio muhimu kwa uchukuzi wa meli na mafuta unaweza kuvivutia vikosi vya wanamaji wa Marekani na vilke vya angani.
Graphic showing military balance between Saudi Arabia and Iran
Presentational white space
Kwa kipindi cha muda mrefu, Marekani na washirika wake wameona Iran kama taifa ambalo halitaki amani kudumu katika eneo la mashariki ya kati .
Uongozi wa Saudia pia nao unaliona taifa hilo kuwa tishio na mwanamfalme huyo anaonekana yuko tayari kuchukua hatua yoyote kukabilisha na ushawishi wa Iran unaozidi kuongezeka.
Hatari ni kwamba vitendo vipya vya Saudia vinazidi kulifanya taifa hilo kuonekana kuwa chanzo chengine cha mgogoro katika eneo hilo.


Comments

Popular posts from this blog

FAIDA ZA KUOA MKE ALIEKUZIDI UMRI

HISTORIA YA KHALIFA WA PILI SAYYIDNA OMAR (R.A)

Elimu kwa wanawake