Posts
- Get link
- X
- Other Apps
KAKA wa mwanamuziki maarufu Nasibu Abdul ‘Diamond’, Romeo Jones ‘Romy Jons’ amefunguka kuwa katika kitu ambacho hawezi kukifanya ni kumsaliti mke wake kwani anampenda sana hivyo kufanya hivyo kutamuuma sana. Romy alisema kuwa, huko nyuma angeweza kusema anahangaika kwa vile ujana unamsumbua lakini kwa sasa hivi ametulia sana na anamuomba Mungu kila kukicha amlindie ndoa yake. “Kitu ambacho namuomba Mungu siku zote shetani tu asiniingie nikamsaliti mke wangu maana hiyo itaniumiza sana kwa sababu nampenda na sitaki kumkosea kwa dhambi ya usaliti hata kidogo,” alisema Romy. Romy alifunga ndoa na mkewe Kahuye Jord ‘Kay Jord’, Desemba 1 mwaka 2017 ambapo baadaye aliangusha bonge la sherehe katika Ukumbi wa Cardinal Rugambwa maeneo ya Oysterbay jijini Dar na kuhudhuriwa na mastaa kibao.
KAMA HUKUOA MKE ZAIDI YA MMOJA MBARONI HUKO USWATINI KWA MSWATI
- Get link
- X
- Other Apps
MFALME ATOA AMRI VIJANA WAOE WAKE KUANZIA WAWILI Mfalme wa King eSwatini amewataka vijana wote nchini humo waliofikisha umri wa kuoa, kuoa haraka huku akisisitiza kuwa wanatakiwa kuoa wake walau kuanzia wawili na kwa wale watakaoshindwa kufanya hivyo watafungwa jela ifikapo june 2019. Mfalme huyo ambaye anawake 15 na watoto 25 na inaelezwa baba yake alikuwa na wake zaidi ya 70 na watoto 150, amesema nchi ya eSwatini inakabiliwa na tatizo kubwa la wanawake kukosa waume kutokana na nchi hiyo kuwa na wanawake wengi kuzidi wanaume. Nchi hiyo ambayo inaaminika kuwa na ‘mabikira’ wengi swala la ndoa za wake wengi limekuwa likionekana nikitu cha kusifiwa licha ya kuwa familia nyingi zikishi kwenye maisha ya kawaida
SUGU APATA MTOTO AMPA JINA LA J-Z
- Get link
- X
- Other Apps
MBUNGE wa Mbeya mjini (Chadema), Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ na mchumba wake, Happyness Msonga wamefanikiwa kupata mtoto wa kiume ambaye wamempa jina la rapa maarufu wa Marekani, Shawn Carter maarufu kama Jay Z. Sugu ambaye pia ni rapa mkongwe hapa Bongo, ametumia ukurasa wake wa instagram kuandika maneno haya. “Tumempa mtoto wetu jina Shawn joseph Mbilinyi… SHAWN (Tamka SHON), lina maana ya zawadi kutoka kwa Mungu ( A GIFT FROM GOD). Pia ni katika kumuenzi msanii na mfanyabiashara maarufu duniani JAY-Z, ambaye jina lake halisi ni SHAWN CARTER. Hii ni kutokana na jinsi FALSAFA zake kuhusu HUSTLING zilivyonisaidia kufika hapa nilipo kwenye maisha. Asanteni sana… # JONGWE # MVMP # MisutiKabatini ,” ameandika Sugu.